• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Biden: Oktoba 15 Mdahalo Usifanyike Kama Trump Bado ana COVID-19

#1

Mgombea wa urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden amesema mdahalo wa pili wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 15 haupaswi kufanyika kama bado Rais Donald Trump atakuwa na virusi vya corona.
Biden amewaambia waandishi habari kwamba yuko tayari kushiriki katika mdahalo huo, lakini kama itabainika Trump bado anaugua COVID-19 jambo hilo halipaswi kufanyika.
Amesema hajui hali ya Trump inavyoendelea, tangu rais huyo aliporejea kwenye Ikulu ya Marekani, baada ya kulazwa kwa siku tatu kwenye hospitali ya kijeshi ya Walter Reed baada ya kuambukizwa virusi vya corona.
Mdahalo wa tatu wa urais nchini Marekani umepangwa kufanyika Oktoba 22. Mapema jana, timu ya Kampeni ya Biden, ilisema mgombea huyo hana virusi vya corona.