• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Bila Kujiongeza Maisha Haya Huwezi Kumove on Katika Maisha Kama Kijana

#1
Moja Kati ya vitu nilivyovigundua katika maisha haya ni kwamba

1. Ukisubili upate kazi ndiyo uweze kuanza maisha utachelewa sana .
2. Ukisubili upewe mtaji na wazazi au ndugu zako wa karibu ufanye biashara utachelewa sana
3. Ukisubili marafiki zako wa karibu wakusaidie kupata kazi au kukupa fursa utachelewa sana .
4. Ukisubili wazazi au ndugu waliofanikiwa ndio waamue hatma ya maisha yako utachelewa sana


Katika haya maisha nilichogundua bila kujiongeza kijana mwenzangu hakuna mtu atayetokea kuja kukusaidia kutatua changamoto zako zinazokukabili bila wewe kujiongeza ninaposema kujiongeza hapa nina angalia maeneo Makuu matatu eneo la kwanza kujitegemea
eneo la pili plan ipi utatumia kuendesha maisha yako ya kila siku
eneo la tatu kutengeneza familia yako ya

Nikianza na eneo la kwanza kujitegemea kijana unapoanza kufikiria kujitegemea ndipo akiri inapoanza kukuaa ufahamu wapi pakuanzia

Eneo la pili ni plan ipi utatumia kuendesha maisha yako ya kila siku hapa nina maana kama kijana unatakiwa utafute plan ya kuendesha maisha yako kama unaona issue za kazi hazija kaa poa basi karibu biashara au kazi nyingine

Eneo la tatu ni mahusiano familia yako ya badae hapa ninazungumza especially vijana wa kiume kama upo nyumbani ni ngumu kupata mwanamke ambae atakuwa tayali kufanya maisha na wewe kama upo nyumbani bado

Kama una lolote la kuongezea ruksaa