• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Elimu ni Nini? Ni Majengo ya Shule na Vyuo? Vipi kuhusu kujielimisha mwenyewe?

#1
Kwa watu wengi, Elimu imekuwa na maana ya kwenda mahali panapoitwa shule, au Chuo ambako walimu na Wahadhiri huwapatia wanafunzi maarifa kwa miaka na miaka kabla ya kutawanyika huku na kule ulimwenguni. Hebu tuone, mathalani, maarifa ya somo la Historia. Â Nini tunachohitaji katika maarifa hayo?

Je, tunahitaji visa ya miji ya kale na wanasiasa waliokwishakufa?
Je, ni kweli mambo haya ndiyo yanayotujenga kielimu?
Je, kuhifadhi historia tu kichwani ndiyo elimu?
Au je, kusomea tu historia ya mabaki ya kale ndiyo maarifa yenyewe tunayoyahitaji kutoka kwa mwalimu katika majengo ya taaluma?
 Au mafundisho yanayopatikana katika historia ya kale ndiyo tunayoyahitaji?
Kama ni hivyo, je, maarifa haya hatuwezi kuyapata kwa kujitegemea wenyewe?
 Mwanataaluma mmoja mashuhuri aliandika kitabu kuelezea maarifa yake mwenyewe aliyoyakusanya huku na kule. Kitabu kinaelezea yale aliyoyasoma yeye mwenyewe.  Hapa sina maana ya kupuuzia thamani ya elimu inayopatikana shuleni au elimu katika mfumo rasmi (formal education) bali ninachokisema hapa ni kwamba kipawa cha kuyasoma mambo kwa upeo mpana na kwa undani zaidi ndicho hasa kinacholeta maana ya usomi hata bila kukaa kwenye dawati au jengo la shule.  Wakati fulani nilikuwa namsikiliza Jim Weiss, mtaalamu wa mambo ya simulizi za hadithi, akisimulia tukio ya kifo cha Teddy Roosevelt na tukio la Harry Truman kuwa Rais baada yake.  Mtaalamu huyo alielezea wasifu wa Rais Roosevelt, ambaye alitokea katika familia ya kitajiri, na ambaye alipata elimu katika Chuo Kikuu cha Ivy League. Sifa na akili yake vilionekana kuleta mafanikio.  Lakini Umma haukumuona Truman kama mtu mwenye uwezo wa kumrithi Rais Roosevelt kwa namna yoyote ile. Tofauti kubwa kati yao ni kwamba wakati Teddy Roosevelt alisoma Chuo Kikuu, Truman yeye alijielimisha mwenyewe (self-educated).  Alikusanya vitabu na vitabu vya historia na akavisoma na kuvisoma. Yeye, zaidi, alipendelea kusoma historia ya tamaduni za jamii za kale na watawala wake.  Katika mahojiano fulani, Truman alitoa sababu za mafanikio yake makubwa ya kidiplomasia kuwa ni kuzirejea taratibu za jamii zilizofanikiwa katika historia. Alipenda kurejea nyuma na kuoanisha tatizo la sasa la mwanadamu na ufumbuzi wake uliopatikana huko nyuma. Hili ni jambo lililomletea mafanikio.  Lakini, ni wangapi kati yetu tunaovutiwa na historia? Je, tunaelekeza mazingatio katika mafunzo ya historia? Je, tunaitumia historia ya miaka kenda kuyatafakari upya mazingira ya leo? Ni dhahiri hapana! Tunayo shule ya kutosha katika Qurâan na Sunna.  Tukisoma shule hiyo, tutapata elimu kubwa na sahihi ambayo ni yenye manufaa ya kudumu. Tukisoma maneno aliyoyasema Mtume karne nyingi nyuma tutapata maarifa makubwa ya jamii.  Tutaona nini sababu ya Waislamu wakiwemo wanaosoma sayansi ya jamii kushindwa kuinusuru jamii yao na mila na madhara ya mila na tamaduni potofu.  Mtume alishasema, âKwa hakika mtafuata mila za wale wa kabla yenu kiasi kwamba hata wakiingia kwenye shimo la kenge na nyie mtaingia humo.â Ikaulizwa, âje, una maana ya Mayahudi na Manaswara?â Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, akajibu, âkama si wao ni nani tena?â (Bukhari na Muslim).  Tumekuwa wagumu wa kusoma. Qurâan imejaa maelezo mengi ya jamii za wanadamu, makosa na mafanikio yao. Mwenyezi Mungu anayatumia maelezo hayo kutoa nasaha fupi na za wazi juu ya namna bora ya kupata maarifa makubwa yenye manufaa hapa duniani na Akhera.  Hadith nyingi za Mtume, swallallahu alayhi wa sallam zina mambo mengi yanayohusu maisha. Je, mafunzo haya ni magumu kusomeka? Au kwa sababu mawazo yetu yameelekezwa katika mambo mengine?  Tujiulize tunatimiza wajibu gani kama wazazi, raia, majirani, waume, wake, waajiri, waajiriwa, marafiki? Je, dunia ndio ibaki tu kama ilivyo, na tuondoke duniani tukiwa tumeiacha hivi hivi?  Je, tuendelee kusoma na kubukua, kulimbikiza shahada, astashadaha na stashahada kwa ajili ya kupata kazi tu na maisha mazuri? Nini maana ya kusoma ikiwa kazi nzuri haikupatikana? Nini maana ya elimu ikiwa maisha mazuri hayakupatikana?  Je, ni kweli kusoma kuishie kumiliki shahada badala ya kumjua Mungu na kumtukia? Je, kusoma kuishie kujaza CV pasipo kulijua lengo la maisha haya? Je, mwisho wa CV uwe ni kusomwa tu msibani kabla ya mtu kufukiwa udongoni? Je, hatuoni kuwa elimu isiyoambatana na uchaMungu haina nguvu halisi ya kumtimizia mtu hitajio halisi la maisha yake?  Je, tubaki tu kuishi kama wanyama wa kula na kunywa, au tuishi kama viumbe wenye hadhi katika dunia hii na wenye maisha ya kudumu baada ya kifo au tutumie muda wetu kufanya jitihada za kuhimizana kuishi kana kwamba tunakufa kesho? Tusisahau kuwa hali yetu ndiyo itakayoamua mafanikio yetu au kushindwa kwetu katika maisha haya.  Tufanye jitihada za kujielimisha sisi wenyewe na kuwaelimisha wale wanaotuzunguuka kuhusiana na lengo halisi la maisha yetu kama lilivyoelezwa katika Qurâan: âSikuwaumba majini na wanadamu ila wapate kuniabudu.â (51:56)