• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Faida 5 za kuwa na followers wengi katika mitandao ya kijamii (Instagram)

#1

Instagram ni mtandao unao aminiwa na kutumiwa na watu zaidi ya bilioni 1 duniani kote. Hapa nitakuonyesha sababu za wewe kuweza kutumia Instagram na kuwa na wafuasi wengi.
  1. Kukuza biashara yako
Kama nilivyo kwambia awali, Instagram inawatumiaji wengi na Tanzania ni miongoni mwa nchi za Africa zinazo ongoza kuwa na watumiaji wengi Zaidi katika mtandao huo.
Unaweza kukuza biashara yako kwa kutangaza kwa kupost matangazo ya biashara yako. Hapa ndipo unaweza kushangaa na kujiuliza kwanini watu wengi wanaangaika kuhakikisha wanapata followers wengi. Kuwa na followers wengi inasaidi kuwafikia watu wengi na kwa haraka pindi unapo hamua kutangaza biashara yako. Ni dhahili kwamba picha au tangazo la biashara yako litakapo onekana kwa watu wengi basi bila shaka kuna baadhi ya watu wanaweza kuvutiwa na kuhitaji huduma yako. Kuweka biashara yako sehemu ambapo watu hawawezi kuiona wala kuifikia ni sawa na bure. Bonyeza hapa kujifunza namna na jinsi ya kuongeza followers katika Instagram na uweze kukuza biashara yako leo.
  1. Tengeneza pesa kupitia makampuni mengine
Unaweza kutengeneza pesa kwa kupitia makampuni mengine kwa kutangaza biashara au huduma zinazokuwa zinatolewa na makampuni hayo. Baadhi ya makampundi utumia programu za mtandao zinazozojulikana kama Affiliate programs ambapo utapatiwa link kisha unaweza kuitumia katika bio yako ya Instagram na utahesabiwa na kulipwa pindi mtu anapo bonyeza na kufuata link uliyoiweka katika profile yako. Makampuni ya nayotoa huduma hii yapo mengi kama unajisikia na unahitaji kufanya hivyo ili kujiingizia kipato unaweza kuingia katika Google na kisha tafuta ‘affiliate programs. Njia hii ni nzuri na unaweza kufaidika nayo kama utakuwa na followers wengi.
  1. Tangaza biashara za watu wengine
Njia hii ni nyepesi na ya haraka sana ya kutengeneza pesa kupitia mitandao ya kijamii ambapo utapatiwa na mtu mwingine tangazo la biashara yake ambayo anahitaji uitangaze katika akaunti yako. Mara nyingi kama siyo mara zote, mtu hatokubali kulipia tangazo katika akaunti yenye followers wachache. Unapokuwa na followers wengi basi njia hii haihitaji nguvu nyingi kuzunguka ili kupata watu wa kutangaza Katika akaunti yako bali watu wenyewe watakutafuta na kuomba uwatangazie biashara zao.
  1. Kuongeza furaha
Unaweza kuwa na picha nyingi nzuri katika akaunti yako lakini ukawa hauna watu wa kuziona, nadhani hicho siyo kitu kizuri. Inapendeza na kuongeza furaha yako pale unapo post nakuona watu wengi wana furahi na kulike picha zako na hiyo ndio maana halisi ya kutumia mitandao ya kijamii.
  1. Kuongeza uaminifu
Kuwa na idadi kubwa ya wafuasi inaongeza watu kukuamini na kufanya wawe tayari kufanya kazi na wewe.