• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

FURSA ZA BIASHARA: JINSI YA KUZITAMBUA NA KUZITUMIA

Edgar Mbele

Moderator
Staff member
#1
Je unatafuta fursa ? Je unafikiri kuwa maisha yako yangeboreka kama ungekuwa na fursa zaidi ? Kama ndio nina habari njema kwako.
Maana ya Fursa za Kibiashara
Kwanza kabisa acha KUTAFUTA FURSA, kwasababu kufanya hivyo ni kurefusha mchakato wa kufaidika na fursa. Fursa hazitafutwi, fursa hazitengenezwi, kwakua fursa daima zipo.
Nasema fursa zipo daima kwakua maana ya fursa ni tatizo ambalo linahitaji suluhu na kupitia suluhu hiyo huyo mtoa suluhu atafaidika kwa kuingiza kipato au kupiga hatua kwa namna nyingine yoyote.
Ninaposema tatizo namaanisha ugumu wowote ule ambao wewe upo katika jamii. Ugumu huo unaweza kuuona wewe kama wewe hivyo suluhu yako ikasambaa kwa watu wengi zaidi ambao wana tatizo kama lako, au ugumu (tatizo) likawa linawagusa watu fulani wewe ukalitatua kwa ajili yao, na ukaingiza kipato.

Mifano ya jinsi ya kutambua fursa za kibiashara
Ngoja nikupe mifano ya mambo makubwa duniani ambayo yamefanyika kwa kuangalia fursa kwa namna hiyo niliyoitaja hapo juu.
Huduma maarufu ya kuhifadhi taarifa mtandaoni iitwayo DROPBOX ilianzishwa kwakua mwanzilishi wake alikua msahaulifu sana wa FLASH DRIVE. Hivyo akatafuta njia ya kuhakikisha files/taarifa zake zinaweza kupatikana popote pale , hata akisahau flashdrive.
Au chukulia mfano wa YouTube iliyoanzishwa kwa sababu waanzishaji walipata shida ya kutafuta video ya Janet Jackson ambaye aliachia matiti wazi wakati wa show ya Super Bowl, hivyo waanzishaji wa YouTube wakajiuliza laiti ingekuwepo huduma ambapo watu popote pale wanaweza kushare kwa urahisi wao wenyewe videos za watu au matukio mbalimbali pengine isingekua shida kwao kuipata hiyo video ya YouTube.
Mfano wa FURSA iliyoonekana baada ya kutazama tatizo la watu wengine ni huduma ya barua pepe ya GMAIL. Huduma hii ilikuja kwakua ilionekana wakati huo huduma za barua pepe hazikua na namna ya kuwasaidia watu kutafuta emails zilizopita , na pia nafasi ndogo ya kuhifadhi emails ililazimu watu kufuta emails zao nyingi tuu.
Ninachojaribu kusema ni kuwa badala ya kuhangaika KUTAFUTA FURSA, au KUWAAMBIA WATU WAKUONYESHE fursa, anza wewe mwenyewe KUZIANGALIA FURSA. Fursa zipo kila wakati , kila mahali. Unachotakiwa tuu ni umakini wako wa KUTAZAMA na KUUNGANISHA UNGANISHA mambo ili uweze kulitambua tatizo haswa ni lipi na uweze kubuni suluhisho sahihi.

Nini ufanye ukishatambua fursa
Kulitambua tatizo na hata kubuni tuu suluhisho peke yake hakuwezi kukunufaisha kama haujajua vema namna ya kuwasilisha suluhu yako kwa walengwa, namna ya kuchambua soko na kupanga uzalishaji na uuzaji wa hicho utakachozalisha au kusambaza.
Sio lazima utengeneze bidhaa mpya, inawezekana hata kuboresha bidhaa zilizopo tuu ni fursa, au kutoa bidhaa toka eneo moja kwenda eneo lingine.
Mfano wa bidhaa iliyozalishwa kwa kuona fursa ya kuboresha bidhaa iliyopo ni kifaa cha kusikiliza muziki cha Apple kiitwa ipod.

Anza sasa kutumia fursa za kibiashara
--Je umeanza kutambua fursa na unataka muongozo wa jinsi gani ya kuhakikisha kweli inakuingizia kipato ? Njoo tuzungumze. Upate ushauri wa kitaalamu kuhusu utengenezaji wa bidhaa (Product Development) na pia namna ya kuwafikia wateja unaowalenga walipie bidhaa husika. Nicheki hapa FB au kwa WhatsApp +57 301 297 1724