• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

HOUSEGIRL WA DADA - 3

#1
HOUSEGIRL WA DADA - 3
Chombezo : Housegirl Wa Dada
Sehemu Ya Tatu (3)


Bibi yule aliniangalia na kuniangazia miale yake kutoka machoni mwake lakin sikujua ujasili wa kubishana nao ulitoka wapi sikuwez kupanua mdomoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

ulifungwa kabisa hapo aliace alianza kulia huku nilikiwa sina hata dalili ya kula chakula kile!

Baada ya kugoma kula bibi alimwambi alice anirudishe duniani na kusem mrudishe siku nyingine

Alice alinivuta mkono kwa hasira na kuanza kutoka kule chini baada ya dakika kadhaa tulifika nchi kavu na kuelekea nyumbani ilikuwa imeshakuwa saa kumi na moja asubuhi tulifika na alice alinirudisha palepale kitandani kwangu

Nilivyoamka asubuhi nilihisi nimechoka sana na mdomo ulikuwa na dam niliwaza hizi dam nimezitoa wapi lakin alice alikuja na kuniambia usiku umenikera sana umekataa kula chakula cha kwetu kumbe hunipendi na nakuahidi hivi ukitaa tena wakati mwingnie nitamuuwa dada yako na mtoto wake .

Hapo niliwaza na kujisemea nilijua alice ni mchawi kumbe ni jini?

Duuuu hapa kazi ninayo maana kujitoa kwake ingekuwa ngumu sana na niliwaza kumwambia dada siku hio na nilienda na kumuita Dada yangu alivyokuja nilitaka kumueleze matukio yote kuwa alice sio binadamu
Gafla yule bibi alitokea na kuninyoshea kidole tena hapohapo alice alikuja na kukaa sebuleni huku akiniangalia kwa jicho kali sana nilishikwa na kigugumizi cha kuongea
Maana alice yuko sebuleni hataki kutoka na bibi yuko pembeni yangu huku akiwa amesimama niliamua kukaa kimya dada yangu hakuelewa ninemuitia nini na niliinuka na kuelekea chumban kwangu nilpofungua mlango nilikuta hela zimefungwa vizuri zikiwa kitandani kwangu!

Nilivyoingia chumbani kwangu nilikuta burungutu la hela zimefungwa vizuri zikiwa kitandani kwangu hapo sikuweza kuwaza nifanyeje nilizikusany na kuziweka kwenye begi langu

Wakati namalizia kuweka alice alinifuata chumbani kwangu na kunishika bega na alisema unaenda kuwa tajiri sana maana mama yangu anakupenda na ukitka kitu chochote muombe atakupatia

Nilimwangalia na kusema utajili wangu utakuawa wa harali na wahaki sio kama huu wa kupewa!

Alice alitoka pale na kwenda kuendelea na kazi zake nilibaki nimekaa kitandani kwa muda huo Neema ambaye ni mpenz wangu alinipigia Sim na kunisalimia wakati naendelea kuongea Alice alingia chumbani kwangu huku akipitia ukutani

Alinyoosha mkono na kunipora simu huku akisema sitaki uwe na mwanamke mwingine alitoka na kwenda kuendelea na kazi zake!.

Muda wa usiku chakula kiliiva niliitwa lakin nilikuwa sina hamu ya chakula hivyo sikuweza kwenda kula na alice aliahirisha kula.

Niliendelea kulala na usiku wa manane ulivyofika niliweza kustuka kutoka usingizi nilianza kusikia sauti za watoto tena chumbani kwa alice na alikuwa akiongea niliamua kuamka na kunyata kwa ajili ya kwenda kuchungulia

Nilivyofika mlangoni nilifanikiwa kuchungulia na niliona nyoka mkubwa sana imejikunya kitandan kwake hap nilianza kutetemeka na kuanza kutoka pale wakati natoka Dada yangu aliniona

Aliniuliza umetoka kufanya nin chumbani kwa alice sikuweza kuongea kitu nilimvuta mkono na kumpeleka achungulie ashuhudie mwenyew tukio lile
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alifanikuwa kuangalia alikuta nyoka mkubwa sana alishangaa sana maana alikuwa hajui chochote kinachoendelea mle ndani!

Alitoka pale huku haamini alichokiona chumbani kwa alice alijisemea itabid kesho nimrudishe kwao.

Nilifungua mlango na kuingia chumbani kwangu lakin cha kushangaz nilimkuta yule bibi chumbani kwangu na alikuwa amelowa dam kweye nguo zake

Hapo sikufikilia nifanye nin nilistukia nimepiga magoti na kuanza kumuomba mungu aniepushe na dhahama ile niliomba duuuu wakati nilikuwa sijui kuomb lakn siku hio niliweza kuomba aisee

Yule Bibi aliniangalia kwa jicho Kali sana.na mimi sikuweza kumuogopa mwishowe aliondoka bila kunidhuru hapo niliinuka na kuoanda kitandani!

Nilikuwa ata sijamaliza dakika mbili alice aliingia na alininyoshea mkono wake ilitoa miale ndani ya mkono wake alinilegeza sana sikueweza kuwa na nguvu za kuinuka na alinisababishia kuwa bubu kuanzia hapo sikuweza kuongea tena

Na mwili ulilegea sana na sikuwa na uwezo wa kuongea chochote!

Kwa usiku huo nilionja joto la jiwe maana nilikuwa nahisi mwilivwangu unachomwa sindano na kujikuna nilikuwa siwez hivyo nilijuta kuzaliwa

Baada ya muda kadhaa Alice alikuja tena na kusema hiyo ni adhabu ndogo tu inayokuja utajuta kunifaham!

Asubuhi ilifika ikiwa bado niko vilevile na dada yangu aliniita kwa ajili ya kunipa maagizo aliita sana na nilimsikia lakin sikuweza kuitika

Aliamua kuingia chumbani kwangu na kunikuta nimelala nikiwa nimelegea na siongei chochote alianza kujiuliza mdogo wangu kulikoni umekuwa hivi

Alitaka kumuita daktari wake lakin nilitikisa kichwa ishara ya kumkatalia aliamua kutoka nje kwa ajili ya kutafuta msaada zaidi kwa majilani!

Wakati ametoka nje alice alikuja chumbani kwangu na kusema nakurudisha kwenye hali yako ya kawaida ole wako uongee chochote leo nakuua

Alininyoshea tena mkono na nilipata nguvu na kuinuka kitandani nilienda kukaa sebuleni Dada alivyorudi alinimkuta nimekaa sebuleni pale alibaki anashangaa!


baaada ya dada yangu kuingia na kunikuta nimeshaamka alishangaa sana alianza kuniuliza lakin sikutaka ajue maana ningesema ningehatarisha maisha yake na mtoto wake!

Aliniuliza ilikuwaje lakin sikusema na kwaupande wake alianza kumuuogopa alice kuanzia siku hio maana usiku ule alishuhudia nyoka mkubwa kitandani kwake hapo alianza kuwaza kumrudisha nyumbani kwao!

Niliendelea kukaa pale sebulen na alice aliivisha chai mimi nilikataa chakula chake niliinuka na kwenda kula mgahawani nilifika pale nikaagiza chapati tatu na chai ya maziwa nililetewa chapati na kikombe cha chai

Nilivyoanza kumimina badala ya kutoka maziwa zilitoka dam ndani ya chupa nilishangaa sana na nilivyoziangalia chapati nikaona funza wamejaaa nilijiinamia na kuwaza kulikoni nilivyoinuka nilimuona alice mbele yangu akiwa amekaa nilishka na moyo kwenda mbio

Aliniangalia xna alice akasema utakapokuwa popote pale mimi nitakuwepo umezila chakula changu sasa unazidi kuongeza matatizo!

Kwa muda wote ule mama mwenye mgahawa akikuwa akiniangalia aliniona nilivyokuwa nikipumua kwa nguvu akiangalia kinachosababisha mimi kuwa vile hakioni aliamua kuja kunistua wew kijana kulikoni! Nilistukia nimelopoka aliceeeeeeee

Heeeee ndio nani? Aliuliza au umeachwa maana vijana nyie mna mambo mengi
Nikasema hapana mama nistory ndefu unavyoniona hapa nimetoka nyumbani kuna tatizo kubwa sana

Tatizo gani mwanangu!
Nilitaka nianze kuongea nilisikia kibao cha shavuni aliyenipiga sikumuona nilitoka nakimbia hadi nyumbani na sikumlipa yule mama hela yake

niliiingia ndani na kumkuta dada amekaa sebuleni nilipitiliza hadi chumbani kwangu na kukaa kitandani! Dada alinifuata na kuniuliza kulikoni
Nikasema aliceeeeee dada atamiuwa mimiiiiiii

Atakuwa?? Mbona sikuelewi
Utanielewa dada alice siyoooooo!!
Sikumalizia kuongea nguvu zikaisha damu zikaanza kuchuruzika kutoka puani maana nilikimbia sana siku hio nililala kitandani

Hapo dada hakuwa mpole tena ilianza vita kati ya alice na dada yangu
Dada yangu alimuita na kumuuliza kulikoni mbona Clifford yuko hivi na chanzo ni wew naomba uongee vinginevyo Leo utanijua mimi ni nani!

Ongeaaaaaa unamtaka nin mdogo wanguuu! Waliendelea kubishana pale na zikawa fujo majirani walikusanyika na kushuhudia tukio lile mimi nikiwa kitandani nilikuwa siwez kuongea tena ila kusikia nasikia kinachoendelea

Dada yangu alimvuta alice na kumpigiza ukutani hapo aliamsha mashetani yote ya alice alianza kubadilika na kutokuwa na umbo maalum Mara nyoka, Mara mtoto yaani hakuwa na umbo maalumu la kueleweka

Hakika zilikuwa fujo na story nyingine pale mtaani dada yangu aliamua kumpigia simu shemeji yangu na alikuja akiwa na rafika yake alishangaaa sana kukut hali ile pale nyumbani!

Wakati fujo zile zikiendelea alipita mzee mmoja alikuwa anaendesha baiskeli alifika pale na kuuliza kunanini hapa?

Majiran wachache walianza kumumwambua kuwa house girl wa dada huyu ni mchawi na anaonekana kama jini alitaka kumdhuru kijana yule aliyeletwa pale sebuleni

Mzee yule alikuwa anaitwa nzee meshaki aliingia ndani moja kwa moja na kunikuta dam zikiwa zinatoka shemeji alitaka kunipeleka hospital lakin mzee Yule alikataa aliinuk pale na kutoka nje kufungua mzigo wake

Alivyorudi aliludi na bible mkononi na kusema kama kweli huyu kijana anateswa na house girl huyu kuanzia leo uchawi na mashetani yote yatatoka humu ndani aliongea hivyo huku alice akiwa anahasira sana macho yake yalikuw yamebadilika na kuwa kama ya paka na mara yalikuwa meusi

Hapo mzee Meshaki alianza kuomba aliomba sana mzee yule hakika alikuwa anajua kuomba alizidi kuomba sana ndani ya nusu saa alice alilegea na kuanguka chuni

Wakati ameeanguka chini mzee alimfuata pale alipokuwa amelala alice na alimshika kichwa kwa muda ule niliweza kumiona Bibi kizee yule akiwa amesimama mbali na muombaji yule huku akirusha miale yake bahati nzuri mzee aliyekuwa akiomba alikuwa eshikilia bibble hivyo ile miale haikuweza kumfikia mzee yule!

Alice alivyoanguka chini alianza kupiga fujo San kila mtu alishangaa sana na Bibi yule alizidiwa na kuondoka zake alimuacha alice akiwa ameshikiliwa huku akipiga fujo sana baada ya saa moja kupita huku yule mzee meshaki akizidi kuomba.

Alice alizidi kulege na kuanza kuongea kwa kuomba msamaha hapo aliongea vyote alivyokuwa akifanya tangu utotoni na kwa nini alifikia hatua ya kuwa vile!

Na kusema nani aliyesababisha yeye kuwa vile na kupandikizwa jini mwilini mwake!

Alice aliliegea sana na nguvu kumuishia baada ya kuombewa na mzee meshaki ambapo alianza kumuuliza kwa nini unaisumbua familia hii nan alikutuma uje kuisumbua familia hii

Alice alianza kuelezea mkasa wote kwa nini huwa anakuwa katika hali ile na kwa nini huw hali chakula kingi

Alianza kutoa historian ya baba yake kumbe aliweza kumkabidh maswala ya uchawi kipindi ndio yuko darasa la tano tu na alikuwa anauwa vijana wa kiume umri kuanzia kiaka 15 hadi 25

Na pia alisema huwa anauwa watoto wadogo wa kike ambao ndio wamezaliwa hivyo alikuwa ameplan kumuuwa mtoto wa dada yangu na mimi pia

Ila alikuwa akisita kimiuwa kwa sababa familia yake ilipenda niwe mme wake na walitaka nikabidhiwe kila kitu maswala ya utajili maana alisema baada ya kukabidhiwa uchawi alizidi kuwa maarufu kwa kazi yake

hivyo kila sehemu alikuwa anaenda kiasi kwamba ilifika hatua akawa na uwezo wa kuzama chini ya bahari kwenda kuongea na mawakala zake

Na yule Bibi ndio aliyempeleka na yeye chini ya bahari kwa ajili ya kuwa na nguvu kubwa sana na kuitawala dunia kiuchawi na awe na asili ya jini

hivyo alizidi kuelezea jinsi chakula alivyokuwa akikipika na kukileta mezani nakusema alikuwa hapiki, yeyeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

wakati mwingine aliwatumia ndugu zake kuweza kumsaidia kupika lakin walikuwa wanapika wakiwa uchi na kupanga chakula walipanga wakiwa uchi pia

juice wakat mwingine alikuwa anatengeneza juice ya dam iliyochanganywa na mikojo hakika alielezea vitu Ving sana siku hio!

Mzee meshaki alimuuliza unataka mini ndani ya nyumba hii alice alisema namtaka huyu mtoto na huyu kaka maana ndio ilikuwa target yangu niwapate ila huyu mtoto namtaka akiwa amekufa na huyu kaka namtaka awe mme wangu

Mzee meshaki alikemea Mara moja alice alizimia na kupoteza faham ziku hio walimnenyua na kumpeleka chumbani kwa ajili ya kumpumzisha mzee meshaki hakutaka kumuacha alimfuata hukohuko na kuzudi kumuombea


ITAENDELEA