• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

HOUSEGIRL WA DADA - 4

#1
HOUSEGIRL WA DADA - 4
Chombezo : Housegirl Wa Dada
Sehemu Ya Nne (4)

Wakati akimuombea dada yangu alianza kulia maana tulikuwa tunalishwa uchafu na chakula cha ajabu sana kiasi kwamba alisema akipata fahamu tu kesho nampeleka kwao hakuna cha kumsamehe?!
Alice kule chumbani alizidi kuombewa na yule mzee bila kukara tamaa baada ya nusu saa alice alistuka nakushangaa sehemu alipolazwa alitaka kuongea lakin alikuwa bubu kwa muda ule hakuweza kuongea wala kusikia chochote

Mzee meshaki alimuamru alale alizidi kumuombea tena na tena baada kama masaa sita anamuombea tu miale ilianza kutoka machoni na vidoleni kwa alice na sauti na miungulumo ya ajabu ilianza kusikika!!

Sauti za kukili makosa zilisikika mle ndani kila mmoja alishangaa na alice alianza kuinuka na kutaka kukimbia lakin mlango ulikuwa umefungwa

Alimtishia mzee meshaki kuwa atamuuwa lakini hakuogopa alizidi kuomba na sauti zile zilizidi kusikika kama mwangwi chumbani mle aiseee nilishangaa sana maana nilikuwa nimezoea kuona kwenye movies tu!


Baada ya ukimya ule ndani ya chumb kile mzee meshak alitoka kule chumbani na kuja sebuleni huku jasho likiwa linamtoka sana mimi na Dada pamoja na shemeji yangu tulibaki kushangaa tusijue cha kufanya hapo ndipo mzee meshak alituruhus kwenda kumuona Alice!

Nilikuwa wa kwanza kuingia chumbani na nilimkuta amelala kitandani huku hawez kuongea chochote alikuwa bubu kusema ukweli hata kusikia alikuwa hasikiii nilimtikisa alinitazama na kunionesha ishara ya kutaka maji ya kunywa nilimuelewa nilienda kumchotea na kumletea alikunywa maji sana muda muda huo na

hapo alionesha ishara ya kuhisi njaa na alitaka chakula nilitoka na kwenda kumletea ubwabwa alikula kiasi kwamba kila mmoja alimshangaa ulikuwa haijawahi kutoke tangu alipokuja pale kwa dada yangu alibaki kulia kila alipokuwa akinitazama machoni

alitamani kuongea kitu lakin sauti yake ilikuwa haitoki alilia sana baada ya kuombewa na kutulia aliomba nafasi ya kupumzika tulitoka wote chumbani na kumuacha huko mwenyew mzee meshaki alisema tumuache muda wa kuongea ukifika ataongea kila kitu maana amesharudi kwenye hali ya kawaida ya ubinadamu msimuogope!
Siku hio ilinibid mimi kushika usukani pale nyumbani nilifanya shuguli zote za pale nyumbani niliweza kuandaa chakula cha mchana nilimpakulia Alice chakula chake na kumpeleka chumbani kwake nilimuamsha aliamka na kukaa kitandani nilimnawisha lakin kila alipokuwa akiniangalia alikuwa analia sana hadi nikaanza kuogopa tena!

Nilionesha woga lakin alitikisa kichwa kuonesha kwamba nisimuogope nilitoka chumbani kwake nilienda kukaa sebuleni na kuanza kula chakula changu

wakati naendelea kula Alice alitoa sauti na kuanza kuniita clifforddddd niliitika na kukumbia kufungua mlango wake niliingia nilivyomuangalia kitu cha kwanza aliniambia nisimuogope yeye ni binadam kama mim na mimi nilimjibu ata sikuogopi Alice ndio maana nilkuwana wew muda wote kwa nini nikuogope Leo?

Aliniomba nikamletee mmaji ya kunywa tena niliendea na kumletea pale chumbani kwake aliniangalia wakati nimesimama na kuniuliza unafanya nini huko sebuleni?
Nikamjibu Niko nakula
Sawa wrngine wako wapi?
Nnikamjibu wako chumbani kwao
Mmmmmmmh! Wanadili kunifukuza au

Nikamjibu hapana wanamambo yao tu ata usijali huwezi kufukuzwa wew ni mwanafamilia .

Aliinama nakuanza kujutia hali ile aliyokuwa nayo alianza kuongea baadhi ya maneno ya kumlaumu baba yake mzazi nilimnyamanzisha sana hadi chakula changu kilipoa siku hio

baada ya muda kidogo Dada yangu aliniita na kuniuliza Alice ameanza kuongea niakamjibu ndio ok .
Sasa mwambie akipumzika na usingizi ukiiisha aje sebuleni baadae nitakuwa na maongezi nae itabidi wote muwepo!
Nikasema swa Dada!

Hapo sister aliondoka zake na kutuacha wawili nyumbani lakini Alice alilia sana na kujutia hali ile aliyokuwa nayo

nilikaa nae karibu sana maana nilihisi atajiua na nilimuomba azidi kumuomba mungu.

Nilitaka kutoka nje lakin alinishika mkono na kusema anataka kukaa na mimi nikasema hapana ngoja nikafanye kazi huko nje au twende wote alikataa niliamua kuondoka nje na kufanya shuguli zangu baada ya kumaliza nilikaa sebuleni mwenyewe

Alice alikuja na kukaa karibu yangu na kuanza kuniongelesha

Clifford naomba usiniogope tena mimi ni binadam kama wew ile hali imeshanitoka maana kipind kile nilikuwa nawaza kuua tu muda wote na kufanya vitu vya ajabu sasa najiona Niko sawa!

Oooooh Usijali Alice mimi ni binadam siwez kukuogopa usilie tutazidi kukupenda sana ila nilianza kumuuliza maswali kadhaa na alinijibu vizuri sana

Hivi Alice hio hali ilianzaje hadi kufikia hatua ya kuwa hivyo maana ulikuwa unatisha ulikuwa unanichukua na kunipeleka sehem mbaya Mara baharini na tulikuwa tunapaa kwanini lakini ulikuwa unatufanyia vile..

Alianza kunijibu na kusema Clifford ni story ndefu sana .mimi nilianza kufanya hiz kazi nikiwa na miaka mitano maana tulikabidhiwa na baba yangu mimi na Mdogo wangu aitwaye Salehe ila yeye alikataa

mimi nilivyoanza kukataa baba alinilazimisha sana na nilianz kupatwa na ugojwa wa kifafa ulinitesa sana na nilikuwa naanguka Mara kwa mara na kila usiku ukifika baba alikuwa anakuja na watu wake kuja kunichapa kila siku nilikuwa naamka na alama za fimbo na nilihisi maimivu sana

hivyo nilizidi kuteswa sana kipindi hicho kwa upande wa kaka yangu salehe yeye alikuwa mkubwa aliondoka nyumbani kuanzia kipindi hicho hadi Leo sijui yuko wapi.

Nikamuuliza tena hivo kwa kipind chote hicho mama yako alikuwa wapi? Alice

Daaaaaaa Clifford naweza kusema mchawi huwa hana huruma hata kidogo baba yangu alimfanya kichaa mama yangu kisa alikataa kufanya anavyotaka yeye hapo aliamua kumfanya kichaa mama yangu hadi leo mama yangu nikichaa huko kijijin kweti usagara!

Ooooooh pole sana alice na baada ya kuteswa na baba ulichukua jukumu gani alice?

Clifford kulingana na kuwa nilikuwa mtoto mdogo niliwaza hali yangu ya kuanguka kila siku na has a nikiwa shule niliamua kukubali kuchukua vile vitu ile niwe salama

na hapo baada ya kukubali nilichukuliwa usiku huo na kupelekwa kuapishwa na wachawi wenzake na walifanya sherehe ya kunikaribisha usiku huo hapo ndipp niliakadhiwa tunguli na kupewa mashart ya Nazi hio

hapo ndip ilikuwa Mara yangu ya kwanza kula nyama mbichi na kunywa dam nilianza kupewa nguvu za ajabu sana

Duuuuuiiiiii! Pole sana alice ! Asante Clifford

sasa baada ya kupokea huo uchawi ugonjwa wako uliisha na ulipewa jukumu gani la kufanya Kama mgeni wa hayo mambo!

Kusema ukweli ugonjwa uliisha kuanzia hapo nilikuwa sianguki tena na nilipewa jukumu la kuuwa watoto wadogo kwa muda huo nilikuwa nauwa kuanzia mtoto wa siku moja hadi miaka mitano

na mtoto wa kwanza kumuuwa alikuwa rafiki yangu wa kike nilimuuwa na nilichukua mwili wake na kuupeleka kwa baba kimiujiza wazazi wa yule mtoto walilia san lakini Mimi sikujali hilo!
Maana nilianza kuwa jasili wa kuua na kuanzia hapo nilipewa zawadi na wachawi wa baba nilipewa nguo nyeusi na kufanyiwa sherehe!

Alice alianza kuelezea matukio huku akiwa analia sana na aliniambia aliweza kupewa zawadi na kupandishwa daraja maana alionesha ujasiri wa kuuwa mtu mapema sana hivyo aliongezewa nguvu zaidi na kupewa jukumu la kuanza kutafuta wavulana wenye umri wa miaka 15 hadi 25
Duuuii alice pole sana maana sio kwa shida hizo ulizopitia .

Asante Clifford ndio hali halisi ya maisha niliyopitia acha hayo matukio tukio lililonisikitisha zaidi ni mimi kuambiwa na baba yangu kulala na maiti hilo nitukio lilinifanya niadhirike kichwani hadi leo nilikuwa nafanya matukio yote kakini tukio hilo liliniuma sana!


ITAENDELEA