• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Huenda Unayemwita ‘Baba’ Si Baba Yako! | Mimba Nyingi Ni Majumba Mabovu

#1
Kama kuna ukweli unaouma ni kugundua baba uliye naye si baba yako au mtoto uliyenaye si wako! Hulka ya Watanzania kuwa na mahusiano ya watu wengi imekua kwa kasi kiasi kwamba vinasaba (DNA) vinaonyesha ukubwa wa tatizo. “Aidha 44% ya wanaume wa Kitanzania wanabambikiwa mimba ambazo si zao”. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za mkemia mkuu wa Serikali.

Watu wamekuwa na migogoro mbalimbali ya kimahusiano na pengine inayohusiana na watoto hivyo hulazimika kutoa utata kwa kufanya utafiti wa kisayansi ambao umeonyesha ukubwa huo wa tatizo. Si ajabu yule unayedhani ni baba yako asiwe na yule unayedhani ni mwanao asiwe! Hali hii hakika inaumiza kila pande yaani kwa mtoto na baba iwapo itangundulika hasa baada ya muda mrefu kupita. Hii inatokana na hulka ya kutokujivuna kulea watoto wa wengine au majigambo ya baadhi ya wanaume; niliwahi kusikia kauli hii, “…hana mume pale ana bwege,wanaume tunamtia mimba mkewe yeye analea…”

Aidha sidhani kama kauli hii akiisikia mlengwa atajisikia vizuri kwa sababu huonyesha dharau na kupuuzwa. Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kumfanya mwanamke akubambikie mimba. Sababu hizo ni:

  1. Ndoa: Kama mwanamke yupo katika ndoa na akawa na mahusiano nje ya ndoa kwa sababu zake, unaweza ukabambikiwa mimba.
  2. Ukata: Wakati fulani mwanamke anaweza kupata mimba katika mazingira magumu sana na akaamua kuchagua mwanaume mwenye kipato ili akidhi malezi ya mtoto huku akijua dhahiri yule mwanaume si baba wa mtoto.
  3. Ubakaji: Wapo wanaoweza kubakwa na kwa aibu wakaficha uharamia huo na kuwabambikiza wanaume wengine ili wasiachwe.
Hizi zinaweza kuwa ni sababu kadhaa japo upo uwezekano wa uwepo wa sababu nyingine zaidi ya hizi ndogo ndogo. Upo uwezekano wa mwanamke kugundua kwamba ana mimba iwapo atapima mkojo siku 3 mara baada ya kunasa mimba. Lakini upo uwezekano wa kugundua mimba kama ni yako au si yako iwapo utahesabu siku mlizokutana na siku za mwanamke za mzunguko wa damu.

Utajuaje?
Kawaida mwanamke anatakiwa kuwa na mzunguko imara wa siku 28 labda awe na hali isiyo ya kawaida au mzunguko usio imara.

  • Siku ya 1 – 3/5/7 zinaweza kuwa ni siku za mwanamke kutokwa damu ya mwezi.
  • Siku ya 4/6/8 – 10 ni siku ambazo mwanamke anaweza kukutana na mwanaume na asipate mimba.
  • Siku ya 11 – 17 ni siku ambazo mwanamke anaweza kushika mimba. Aidha siku ya kushika mimba ni moja tu hapo yaani siku ya 14 ambayo mara zote yai la mwanamke hupevuka na kama hajakutana na mwanaume, yai litaharibika na mwisho wa mwezi atatokwa damu tena.
  • Siku ya 18 – 28 ni siku ambazo mwanaume anaweza akakutana na mwanamke na asimpe ujauzito. Baada ya hapo mzunguko huanza upya.
Namna Ya Kuapata Mtoto Wa Kiume Au Wa Kike
Kila mtoto ana thamani sawa lakini kumekuwa na hulka ya watoto wa kiume kupendwa zaidi na pande zote. Mama anaweza kutaka mtoto wa kiume ili amfurahishe baba na baba anaweza kutaka mtoto wa kiume ili ajigambe. Hakuna sababu za msingi sana japo wengi wanasema ukizaa watoto wa kike pekee uzazi wako unapotea kwa sababu wao wataenda kuolewa na hutakuwa na mwendelezo wa jina lako! Pengine hii ni sababu kubwa inayowachagiza wanaume wengi wapende kuwa na watoto wa kiume.

Kuna njia rahisi ya kuchagua mtoto wa kumzaa iwapo mwanamke ana mzunguko imara yaani usio badilika badilika sana. Siku ya 14 ya mzunguko wa mwanamke ndio siku ambayo yai huwa limeiva kwa mwanamke na likipata mbegu za kiume, mwanamke huyo atanasa mimba. Mbegu za kiume huwa zina chembe za XY na mwanamke ana XX.

Aidha mbegu zinazochagiza mtoto wa kiume hukimbia haraka sana zikiingia ukeni zinapokimbilia yai la kike lakini hufa haraka sana, mara nyingi si zaidi ya saa 6. Mbegu zinazotunga mtoto wa kike huogelea taratibu kuelekea kwenye yai lakini zina maisha mrefu karimu saa 72. Iwapo mwanaume atatembea na mwanamke siku ya 11 ya mzunguko, hakika si rahisi mwanamke kutunga mimba ya mtoto wa kiume lakini mbegu za kike zinaweza kukaa kwa siku tatu yaani siku ya 11,12 na 13 na kuja kuingia katika yai siku ya 14!

Na ukitaka mtoto wa kiume, basi hakikisha mke wako ana mzunguko imara na mhesabie siku 13 na ile ya 14 fanya naye ngono bila kinga unaweza ukabahatika mtoto wa kiume. Aidha mtoto ni mtoto, wala usibague kwani unaweza kufurahia mtoto wa kiume akaishia kuwa shoga au ukampuuza binti yako akaja kuwa ‘first lady.’ Thamani ya mtoto haipimwi kwa jinsia bali hupimwa kwa uhai wake, mwanao anapokuwa hai ndipo unapoona thamani ya kuwa naye. Vipo vipimo kwa sasa vinavyotumika kumpima mwanamke kama siku hiyo yai lake limepevuka, unaweza ukavitumia vipimo hivyo kuthibitisha kama kweli mkeo yuko katika ‘joto’!

Kwa Nini Mzunguko Unaweza Usiwe Imara?
Matumizi ya madawa makali ndani na nje ya mwili yanaweza ksababisha mwanamke kukosa mzunguko imara na pia lishe duni. Watanzania wengi hatuli vizuri ni dhahiri Watanzania wengi wana utapiamlo. Pia msongo wa mawazo au maradhi yanaweza kuharibu mzunguko wa mwanamke.

Hitimisho
Tatizo lipo tena kubwa, 44% ni kubwa sana kwa familia kuvurugana kwa sababu ya kubambikiziana mimba. Ni vizuri mwanaume akafuatilia sana mzunguko wa mkewe kila mwezi ili kuepuka majumba mabovu!