• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Idris Afunguka Ugomvi na Wema!

#1


MCHEKESHAJI maarufu Bongo ambaye ni Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa (BBA) 2014, Idris Sultan amefunguka juu ya kile kinachodaiwa kuwa ana ugomvi mzito na aliyewahi kuwa mpenzi wake (eksi), Wema Isaac Sepetu. Idris amesema kuwa, hakuna ugomvi wowote kati yake na Wema ambaye ni staa wa Bongo Movies.Hayo yamekuja baada ya hivi karibuni, mchekeshaji huyo kuandika mtandaoni maneno yaliyoashiria kumlenga moja kwa moja Wema, jambo ambalo liliibua minong’ono mingi kwa baadhi ya mashabiki wao.Ili kujua sakata hilo kinagaubaga, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limemsaka Idris ili aeleze anachokijua, ambapo kwa upande wake, anasema kuwa, hana tatizo na mwanadada huyo na anamheshimu mno;

IJUMAA WIKIENDA: Mambo vipi Idris?

IDRIS: Poa niambie…

IJUMAA WIKIENDA: Safi tu, hivi tangu ule ujauzito wako kwa Wema uharibike, ndiyo huna mpango tena wa kutafuta mtoto mwingine?

IDRIS: (Anacheka) Kusema ukweli tangu kipindi kile aisee, nimekuwa nina-focus sana kwenye kazi zangu.IJUMAA WIKIENDA: Ndiyo kusema bado hujampata mwanamke wa kufanana na Wema au?

IDRIS: Hapana, tangu mimi na Wema tumeachana, nimeshakuwa kwenye uhusiano na wanawake wengi tu, lakini sasa hivi nimeamua kufanya kazi sana kuliko kuweka muda wangu mwingi kwenye hayo mambo.

IJUMAA WIKIENDA: Hivi karibuni mlijibizana na Wema mtandaoni, jambo lililosababisha baadhi ya mashabiki wenu kuhisi labda mna bifu, unaweza kutuambia tatizo hasa ni nini?

IDRIS: Mimi sina matatizo kabisa na Wema, ninamheshimu sana kuliko hata mnavyofi kiria, nilichokifanya ilikuwa ni sehemu tu ya ucheshi wangu na siku zote mimi na yeye (Wema) huwa tunataniana, hivyo ni mambo ya kawaida. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, hivi karibuni, Idris alimuandikia Wema;

“Ushauri tu, kama wewe mwembamba sana, jitahidi usivae wigi kubwa, ukisimama sekunde 30 bila kusogea, watu wanaweza kudhani ni mop (aina ya fagio la kusafi sha buibui ndani ya nyumba).”

Kwa upande wake Wema, naye alijibu mapigo; “Una…(tusi) mwingi na sijapenda, siyo kila kitu utani, it’s not even funny, ningekuwa na mamlaka ningekuweka ndani, ndiyo maana unatiwagwa ndani.”

Enzi wawili hao wakiwa wapenzi, walikuwa wakipendana kama makinda ya njiwa, lakini sasa wanaonekana wazi hawaivi chungu kimoja.#WASANII Wanachuo forums