• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Jeuri ya Fedha… Bella Aibuka na Mjengo wa Kifahari

#1
MWANAMUZIKI mtanashati mwenye sauti ya kinanda Christian Bella ‘Obama’, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ameonesha jeuri ya fedha, baada ya kuibuka na mjengo mkali wa kifahari, Risasi Mchanganyiko limefichua.Uchunguzi na vyanzo vyetu umebaini kuwa, Bella au unaweza kumuita pia ‘Mfalme wa Masauti’, ameotesha mjengo wa maana eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam, mahali ambapo ukitaka kiwanja tu, unapigwa milioni mia. Ukipewa ubuyu usiuamini, uchimbe kwa kina; ndivyo waandishi wetu walivyofanya baada ya kupenyezewa taarifa kwamba, jamaa ‘siyo mwenzetu’ walifika nyumbani kwa Bella na kugonga geti.BONGE LA MJENGO NA SIYO KIBANDA

Japokuwa waandishi wetu hawakufanikiwa ajili ya kuogelea. Wakati waandishi wakitia timu nyumbani kwa mwanamuziki huyo, mwenyewe hakuwepo, lakini dada wa kazi ndiye aliyewakaribisha ambapo walipiga naye stori mbili tatu muhimu.Baada ya salamu za “hujambo kuingia ndani, lakini waliweza kupepesa macho na kujionea uzuri wa nyumba hiyo ya ghorofa moja yenye eneo kubwa la kupaki magari, mandhari nzuri ya kuvutia, pamoja na swimming pool kwa na hapa ndiyo kwa Bella” naye kuitikia ndiyo; waandishi wetu walisepa kwa sababu hawakuona haja ya kumuuliza mambo mengine yanayohusu umiliki wa Bella kwenye nyumba hiyo.MAJIRANI WAFUNGUKA

Mbali na hilo, waandishi wetu waliweza kuzungumza na baadhi ya majirani wa msanii huyo, ambapo waliweza kufunguka kwa upande wao na kuthibitisha kuwa, Bella anamiliki nyumba eneo hilo.“Hii nyumba ni ya Christian Bella na hana muda mrefu tangu amehamia kwa sababu, ilikuwa inatengenezwa ila kwa sasa anaishi hapa na hata ukiangalia hapo nje, utaona kuna gari lake limepaki,” alisema jirani mmoja ambaye hakupenda kutajwa jina gazetini.BELLA YEYE ANASEMAJE?

Risasi lilimvutia waya mwanamuziki huyo, lakini simu yake haikupatikana, ambapo taarifa zilidai kuwa, yuko nje ya nchi kikazi.Hata hivyo, Bella ambaye umaarufu wake umezidi kuongezeka siku hadi siku tangu alipoletwa nchini na mwanamuziki mwenzake wa Kongo, King Dodoo kufanya kazi ya muziki Bongo, amewahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari kuwa, anamiliki nyumba mbili za ghorofa.Pekuapekua yetu imeonesha kuwa, nyumba ya pili bado haijakamilika na kwamba, nayo ni ya ghorofa na ipo mita chache kutoka pale anapoishi.NI SOMO KWA WASANII WA BONGO

Jeuri hiyo ya fedha aliyoonesha Bella kwa kuibuka na mjengo mkali, ni somo tosha kwa wasanii wa Bongo, ambao baadhi yao wakizikamata fedha, huishi kula bata huku wakiendelea kuwaamkia wamiliki wa nyumba walizopanga.Uchunguzi unaonesha kuwa, mastaa wengi Bongo wamekuwa wakihusudu maisha ya matumizi ya hali ya juu na kujisahau kufanya uwekezaji, jambo ambalo wengi wamekuwa wakiishia kubaya baada ya sanaa kuwapiga chini.#Wasanii Wanachuo forums