• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Jifunze jinsi ya kulipia bidhaa mtandaoni

#1

Mara nyingi siku hizi umekuwa ukisikia kuhusu kulipia bidhaa mtandaoni (Online) lakini mara zote umekuwa ukipuuzia labda kutokana na kushindwa au kutokufahamu namna na jinsi ya kufanya ili kulipia bidhaa hizo.
Ni rahisi sana, leo nitakuonyesha namna ya kulipia bidhaa unayoipenda online. Kabla sijaanza kukuelekeza labda nikuombe kitu kimoja, husije ukawa mlevi sana wa hiki kitu, maana utakapo zoea utatamani mambo yako yote umalizie online.
Haraka haraka ngoja nianze kukushushia hatua ambazo utazifuata ili uweze kukamilisha malipo yako ukiwa online / mtandaoni. Tafadhali soma mpaka mwisho
Ili uweze kutumia au uweze kununua bidhaa mtandaoni nilazima uwe umejiunga na kujisajili na huduma ya Online payments. Fika katika bank au tawi la bank yoyote unayohitaji kuitumia kisha omba wakuunganishe na huduma ya Online payments. SHUKRANI SANA kwa makampuni ya simu za mkononi, sasa hauhitaji kwende katika Mabank kwajili ya kujisajili kutumia huduma ya Online payments, sasa unaweza kumaliza kila kitu hapo hapo ukiwa na simu yako ya mkononi.

Nitatumia mfano Vodacom kama moja ya makampuni ya simu yanayotoa huduma hiyo, ila pia katika makampuni mengine jinsi na namna ya kufanya inaweza ikawa sawa.
Katika simu yako yenye laini ya Vodacom fanya yafuatayo:-
 1. Tengeneza kadi yako ya malipo yani M-Pesa Master Card. Jinsi ya kutengeneza bonyeza * 150 * 00 # > Chagua nambalipa kwa M-pesa >Chagua namba 6.M-Pesa Master Card > Chagua namba 1.Tengeneza kadi.
 2. Baada ya kutengeneza kadi utapokea ujumbe ambao utakuwa na vitu vitatu muhimu mamba ya kadi, namba ya CVV pamoja na tarehe ya kadi yako kuisha muda wake.
 3. Sasa rudi katika M-Pesa na uweke kiasi cha fedha unachotaka kutumia katika kadi yako. * 150 * 00 # > Chagua nambalipa kwa M-pesa >Chagua namba 6.M-Pesa Master Card > Chagua namba 3.Weka pesa kwenye kadi
 4. Hapo utakuwa umemaliza sasa hatua inayofuata ni kulipia bidhaa yako.
Nalipia bidhaa gani Online? Unaweza kulipia mtandaoni huduma na bidhaa kibao kupitia kadi yako ulioyo tengeneza. Mfano kununua vitu mtandaoni kama vile mavazi, chakula na kulipia huduma mbalimbali kama vile usafiri wa mabasi, ndege, kununua programu za kompyuta, simu n.k. kununua vifaa kama vile TV, jokofu,kompyuta n.k.
Jinsi ya kulipia
 1. Nenda katika mtandao wowote duniani unaotoa huduma unayohitaji kulipia
 2. Chagua huduma unayotaka kisha chagua njia ya kulipia (Payment Method)
 3. Mitandao mingine kama siyo yote watakutaka utengeneze akaunti na kujaza baadhi ya taarifa zako ambazo baadae zitakusaidia kupata mzigo wako unaotaka kulipia.
 4. Baada ya kumaliza kujaza taarifa zako basi unaweza kuchagua njia ya kulipia. Chagua Master Card. Baadhi ya mitandao hawatakutaka uchague njia ya kulipia, watafahamu mara moja njia unayotaka kutumia kukamilisha malipo pale utakapoanza kuandiaka namba mbili tu za kwanza za kadi yako.
 5. Andika vizuri namba yako ya kadi kama ulivyo pokea katika ujumbe wa simu wakati unatengeneza kadi yako. Kama umefuta kimakosa fanya hivi kuipata tena, bonyeza * 150 * 00 # > Chagua nambalipa kwa M-pesa >Chagua namba 6.M-Pesa Master Card > Chagua namba 2.taarifa za kadi kisha utapokea ujumbe ukionyesha namba yako ya kadi, namba ya CVV pamoja na tarehe ya kadi yako kuisha muda wake.
 6. Andika namba ya CVV na tarehe ya kadi yako kuisha muda yani mwezi na mwaka.
 7. Angalia na bonyeza sehemu inayokutaka ukamilishe malipo yako.
 8. Utapokea ujumbe ukionyesha kufanyika kwa malipo yako kutegemeana na taarifa ulizo jaza wakati unafanya malipo.
 9. Hapo utakuwa umemaliza.
ONYO
 1. Hepuka kuweka kadi yako ya malipo katika mitandao isiyo aminika. Kuwa huru kutumia na kufanya malipo katika mitandao inayo aminiwa na kutumiwa na watu wengi.
2. Husimtumie au kumuonyesha mtu yeyote taarifa za kadi yako. Mtu yeyote anaweza kufanya malipo yake binafsi kwa kutumia taarifa za kadi yako.