• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Jifunze Kuhusu Umuhimu na Athari za Upungufu wa Madini Chuma kwa Watoto

Wanachuo Doctor

WF Doctor
Staff member
#1
UPUNGUFU WA MADINI YA CHUMA KWA MTOTO

Madini ya chuma yaliyopo kwenye maziwa ya Mama hunyonywa vizuri zaidi yale kwenye vyanzo vingine. Vitamin C na kiasi kikubwa cha lactose kwenye maziwa mama husaidia kunyonywa kwa madini ya chuma kwa urahisi sana.

Watoto wanaonyonya maziwa ya mama hawapotezi madini ya chuma wakijisaidia. Maziwa ya ng’ombe yanaweza kuuletea madhara utumbo mwembamba wa mtoto na kusababisha choo chenye damu pamoja na upotevu wa madini ya chuma kwani utumbo mdogo ndio unanyonya madini hayo.

Pia ukosefu wa madini ya chuma ni kati ya sababu za mtoto kupoteza hamu ya kula.

JE, NI WATOTO GANI WANA HATARI KUBWA YA KUPATA UPUNGUFU WA MADINI YA CHUMA?

Watoto waliozaliwa njiti. Pia kuna utafiti unaonyesha watoto waliozaliwa na uzito chini ya kilo tatu (3) hupata tatizo hili. Watoto waliozaliwa na mama wenye kisukari ambao hawana/hawakuwa na uangalizi mzuri/makini wa ugonjwa huo kipindi cha ujauzito.

Watoto waliozaliwa na Mama ambao walikuwa na upungufu wa madini ya chuma kipindi cha ujauzito wana hatari kubwa ya kupata tatizo hili.

Watoto wanaokunywa maziwa ya ng’ombe kama mbadala ya maziwa ya mama au maziwa ya kopo ya watoto ambayo yameongezwa madini ya chuma katika mwaka wao wa kwanza tangu kuzaliwa.

Pia watoto walioanzishwa vyakula yabisi mapema sana wana hatari kubwa ya kupatwa na tatizo hili.

Watoto hupata madini ya chuma kutoka kwenye vyakula vyenye kiasi kikubwa cha madini ya chuma na vitamin C. Kama mama ana wasiwasi na kiasi cha madini ya chuma katika mwili wa mtoto wake basi aonane na daktari ili mtoto afanyiwe vipimo.

Kama mtoto aliumwa karibuni, basi kiasi cha madini ya chuma kwenye mwili wake hupungua kwa muda mfupi lakini hurudia kiasi chake cha kawaida.

DALILI KWAMBA MTOTO ANA UPUNGUFU WA MADINI YA CHUMA

Ngozi iliyopauka na uchovu
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Mtoto kupoteza hamu ya kula.
Ulimi kuvimba au kupatwa na mikwaruzo n.k
Pia mtoto anaweza kuwa na upungufu wa madini ya chuma na asiwe na dalili yoyote ile.

VYANZO VIZURI VYA MADINI YA CHUMA

Wataalamu wanashauri mtoto apewe vyakula ambavyo asilia vina madini mengi ya chuma kuliko vile ambavyo huongezwa madini hayo kiwandani.

Baadhi ya vyakula hivyo ni:
Maziwa ya mama.
Viazi vitamu
Zambarau
Nyama ya ng’ombe, Kuku,Bata Mzinga, Nguruwe, maini ya kuku, ng’ombe.
Uyoga
Mboga za kijani, mchicha, figiri n.k
Nafaka zisizokobolewa (Mtama, Ngano, Brown rice/mchele wa kahawia)
Kiini cha yai.
Maharage, Jamii za kunde
Nyanya na matunda jamii ya machungwa.
Dagaa na samaki
Matunda yalikaushwa kama zambarau kavu, raisins, apricots.

TAHADHARI: Baadhi ya vyakula vilivyotajwa vinaweza kuwa si sahihi kwa mtoto wako.
Ngano, nyama ya nguruwe, samaki, na mayai ni vyakula vyenye hatari ya allergy hivyo umakini mkubwa unahitajika.

Nyanya na machungwa si sahihi kwa mtoto chini ya mwaka mmoja hasa kwa sababu ya kiasi kikubwa cha asidi kwenye vyakula hivyo.

Mengi zaidi yapo katika programu yetu ya My Doctor. Usikose kushiriki katika programu yetu mpya itakayotangazwa karibuni.