• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Jinsi nilivyobadili mawazo ya wazazi wangu…

Edgar Mbele

Moderator
Staff member
#1
Na nikapata kusalia shuleni kwangu!

Wiki chache zilizopita wazazi wangu walinikalisha chini kuniambia ya kuwa walitaka kunhamishia kwenye shule iliyokuwa mbali – ambako ingenibidi kukaa huko usiku wote. Nilipatwa kwa mshangao, sikujua hata niseme nini.

Sababu zao zilikuwa kwamba baba yangu mara nyingi yuko kazini, na mama yangu anafanya kazi masaa mengi siku hizi, kwa hivyo walikuwa na wasiwasi kwamba sikuwa na usimamizi wa mtu mzima nyumbani nyakati za mchana. Ikiwa nilikuwa shuleni ambako ningekaa, ningekuwa na nafasi salama ya kusoma na kutilia makini kazi yangu ya shule.

Nilipitia hisia zote. Nilishtuka (wangewezaje kunifanyia hivi?), hasira (tuligombana na kugombana!), huzuni (sikutaka kuwa mbali na nyumbani) na mwoga (nitawezaje kukabiliana na yote pekee yangu?).

Punde niligundua kwamba hizi panda shuka za hisia nilikuwa napitia hazikuwa zikitatua chochote. Hivyo, nilikaa chini na kufanya orodha ya mbona sikukubaliana na uamuzi wao, na jinsi ningeweza kufanya mambo ikiwa ningekaa nyumbani na katika shule yangu ya sasa.

Niliipeleka kwa wazazi wangu, na tukawa na mazungumzo marefu (wakati huu bila kupaza sauti), na kupima faida na hasara zote. Niliwaelezea kuwa ninafuraha sana shuleni, alama zangu ni nzuri na nina kundi la karibu la marafiki wangu ambao ni wa maana sana kwangu. Niliwaomba pia waniamini nitaendelea kufanya vyema, hata kama mama yangu anafanya kazi hadi jioni. Wazazi wangu walivutiwa sana na jinsi nilivyokabiliana na hali ile. Pia walikubaliana na maoni yangu. Waliona kwamba nilikuwa nimekomaa vya kutosha kutoa maoni yangu na kujisimamia mwenyewe, na walipata ujasiri mpya ndani yangu.

Tulikubaliana kwamba sitahitajika kwenda shule ya bweni, na kama shughul zitaongezeka kwa mama na baba, tutarejelea hali hiyo.

Kwa hivyo, wakati ujao utakapokosa kukubaliana na jambo ambalo wazazi au walezi wako wameamua, kumbuka kuwa una haki ya kuwasilisha maoni yako. Ukikabiliana na hali ile kwa utulivu, ujasiri na kwa wazi, maoni yako yatasikika.