• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Jinsi ya kubadili profile yako kuwa Page ya facebook

#1

Unaweza kuona sio kawaida lakini nataka nikwambie, unauwezo wa kubadili profile yako na kuwa facebook page.
Kuna haja gani ya kubadili profile kuwa page?

 1. Baada ya kubadili utakuwa na profile / akaunti yako kama kawaida na utakuwa na page pia ambayo imetokana na profile yako.
 2. Facebook hairuhusu mtu kufanya matangazo ya kibiashara katika profile ya kawaida. Endepo itaonekana una jihusisha na biashara katika profile ya kawaida basi watakufungia kutumia facebook.
 3. Utaweza kutumia vifaa na mbinu mbalimbali ambazo zimewekwa na facebook ili kukuwezesha kufikia watu wengi.
 4. Utaweza kuona kirahisi idadi ya watu wanao tembelea na kushiriki katika page yako.
 5. Unaweza kubadili marafiki na friends request kuwa wafuasi wako hivyo kuongeza na kuwa na jumuiya kubwa bila kufanya kazi kubwa, kama unavyo fahamu jinsi ilivyo kuwa ngumu kutengeneza jumuiya kubwa katika facebook page.

Hatua za kubadili profile yako kuwa facebook page
 1. Bonyeza hapa kuanza kutengeneza page yako.
 2. Bonyeza Get Started na ufuate maelekezo rahisi kama inavyo elekeza.
 3. Baada ya kumaliza basi utaanza kuweka post mpya n.k
 4. Unaweza kuchagua picha ambazo unaweza kuamishia katika page yako mpya.

Kinatokea nini kwa marafiki, wafuasi, na friend request baada ya kubadili?
 1. Marafiki, wafuasi na walio kutumia maombi ya urafiki watapata taarifa kuwa umetengeneza page nyingine.
 2. Wafuasi ambao utawachagua kutoka katika profile yako watahamia katika page yako mpya.
 3. Marafiki na walio kutumia maombio ya urafiki ulio wachagua wote watakufollow na wata like page yako hapo hapo. Utaona kama una marafiki wengi mfano 2000+ basi utapata like 2000+ hapo hapo na hawata ondolewa katika profile yako ya zamani.