• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

jinsi ya kujitoa kama simu yako imeunganishwa sehemu nyingine (hacked)

Edgar Mbele

Moderator
Staff member
#1
Hiyo inaweza ikawa umeunganishwa katika Call forwarding / call divert. nitakuonyesha namna ya kujiondoa, tafadhali akikisha unasoma mpaka mwisho kabla ya kufanya chochote.
Call forwarding / divert
call forwarding ni kipengele ambacho kipo katika settings za simu yako ambacho kimewekwa makusudi ili kukupa nafasi ya kuamua au kuelekeza simu yako ipokelewe na mtu mwingine ikiwa haujisikii kufanya hivyo.
Mfano uko ofisini, mtu amekupigia katika simu yako akiwa nashida ya kuongea na boss wako ingali hana namba za boss wako, hauna sababu ya kukimbia kumpelekea simu boss wako badala yake unaweza kutumia kipengele cha call forwarding. Kwa maana hiyo call forwarding ni kuielekeza simu yako iweze kupokelewa katika namba / mtu mwingine.
Call forwarding ni kipengele muhimu sana kama mtu atajua matumizi yake na kukitumia vizuri. Husitumie kipengele hicho vibaya kumuunganisha mtu kwa lengo la kutaka ku hack simu zake anazo pigiwa.
Ulishawahi kupokea ujumbe huu kutoka makampuni ya simu
Mteja mwenye namba 075661XXXX alijaribu kukupigia lakini simu haikufanikiwa. Tafadhali wasiliana nae”
Makampuni ya simu utumia kipengele cha Call forwarding ili kukupatia ujumbe huo ikiwa ulipigiwa simu wakati simu yako haipatikani.
Ikiwa simu yako haipatikani basi simu zako zote zitaelekezwa katika kampuni la simu husika kupitia namba maalumu iliyowekwa kwaajili ya huduma hiyo.
Kwasababu namba hiyo imewekwa kwaajili ya huduma hiyo basi mfumo utatambua kuwa namba yako haiko hewani na hapo hapo itatuma ujumbe kukujulisha mtu aliyekupigia kipindi haukuwa hewani.
Jinsi ya kutambua kama umeunganishwa katika Call forwarding
Bonyeza namba hizi kufahamu kama umeunganishwa

Kujua *#62# - kama umeunganishwa utaona namba ulio unganishwa nayo tofauti na hapo utakuwa haujaunganishwa.
Kujitoa ##002# - kama umeunganishwa na unahitaji kujitoa basi bonyeza namba hizo. Kumbuka, kama unatumia huduma ya kutumiwa ujumbe kukutaarifu simu ulizo zikosa angalia namba hizo kwa makini kabla haujajitoa labda kama unahitaji kufanya hivyo, mfano namba +255125 unaweza kuona kuwa sio rahisi ikawa ni namba ya mtu.

Namna ya kuunganisha call forwarding
unahitaji kuzielekeza simu zinazoingia zipokelewe katika namba nyingine? Fuata hatua zifuatazo:-
  1. Katika simu yako nenda katika sehemu ya kupiga simu (Phone)​
  2. Bonyeza Option, katika simu nyingine inaweza kuwa ni alama ya vidoti vitatu.​
  3. Ingia katika call settings.​
  4. Nenda katika Additional settings.
  5. Ingia katika call forwarding.
Fahamu:
Settings za simu yako inaweza kuwa tofauti na za simu ninayotumia. Kitu cha msingi ni kuhakikisha unafika sehemu ya call forwarding.

Weka namba ya simu ya mtu ambaye ungependa apokee simu zako kwa niaba yako katika kipengele ambacho ungependa kukitumia au ondoa namba ya simu kujiondoa.

Katika call forwarding kuna vipengele / machaguo yafuatayo:-
  1. Always forward – simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine na kupokelewa.​
  2. Forward when busy – simu zako zote zitaelekezwa kwenda katika namba nyingine ikiwa simu yako inatumika (busy)​
  3. Forward when unanswered – simu zako zote zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa haujapokea.​
  4. Forward when unreachable – simu zako zote zitaelekezwa katika namba nyingine ikiwa namba yako haipatikani​
Nahisi utakuwa umejifunza na kuelewa vizuri call forwarding. Kama unaswali basi husisite kuuliza, nitakujibu.