• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Jinsi ya kuongeza na kuwa na followers wengi katika instagram

#1

Ni kitu kizuri na chenye furaha sana kuwa na likes nyingi pale unapokuwa unatumia mitandao ya kijamii. Haina maana kama uta post picha yako nzuri lakini hakuna mtu yeyote anaye itazma. Leo nitakuonyesha mbinu rahisi ambayo itakuwezesha kupata na kuwa na followers wengi katika instagram.
Follow unfollow? NO
Najua ulivyoona nimekwambia ntakuonyesha namna ya kuongeza followers tayari ukajua nitakuelekeza kutumia njia ya Follow Unfollow ambayo ni maarufu lakini ni ngumu sana kufanikiwa. Follow Unfollow ni njia inayotumiwa na watu wengi katika instagram ili kuongeza followers ambapo utatakiwa kuwafollow baadhi ya watu ambao baadae na wao watarudia kukufollow (follow back). Kwa njia hii ni kati ya asilimia 10% – 20% tu ya watu ambao wanaweza kukufollow back, kwahiyo unaweza ukaona ni jinsi gani ilivyo ngumu kufanikiwa.
Jinsi ya kuongeza followers wengi katika instagram bila kutumia nguvu
  1. Ingia katika instagram na tafuta akaunti inaitwa @like_my_photo_challenge

like_my_photo_challenge itakusaidia kuongeza followers katika akaunti yako ya instagram, kivipi?
Utatakiwa kuwatumia picha yako moja yenye muonekano mzuri kisha @like_my_photo_challengewataipost na kukutag katika picha yako hapo hapo. @like_my_photo_challenge wana wafuasi zaidi ya laki mbili na kumi (210K Followers) hivyo itafanya picha yako ionekane na kutazamwa na watu wengi ambao watakufuata na kukufollow katika akaunti yako. Ni bure, kwa nini na wewe husijaribu leo?

  1. Mara baada ya @ like_my_photo_challenge kupost, utatakiwa kucomment katika picha yako iliyo postiwa kisha utatakiwa kuwa tag baadhi ya marafiki zako wasiyopungua wa tano (5) ambao ungependa nao wa like picha yako na kukufollow katika akaunti yako. Unaweza ukaona ni kama kitu fulani hakina maana lakini napenda kukuhakikishia kuwa ni kitu chenye nguvu pale utakapo kuwa unaperuzi katika instagram yako pindi unapokuwa unapata chai au chakula cha jioni maana @like_my_photo_challenge haita kugharimu wala kukupunguzia kitu chochote kutoka katika akaunti yako.
  2. Unaweza ukawa shirikisha pia wenzako katika mitandao mingine ya kijamii kwa kushare picha yako iliyopostiwa na @like_my_photo_challenge na itakusaidia tena kuweza kupata likes nyingi zaidi na watu wengi watakufollow pia
  3. Kadri picha yako itakavyo zidi kupata likes nyingi basi @ like_my_photo_challenge wataendelea kuiweka picha yako kwa muda zaidi.
  4. Hakuna kikomo maalum cha kuwatumia picha @like_my_photo_challenge, unaweza kuwatumia picha zako kila siku kisha nao watakupost kadri utakavyo elekeza.
Kwa nini husijaribu leo?