• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Resha Mchanga

CEO & Founder
Staff member
#1
Usajili wa kampuni (BRELA)na masuala mengine mengi kama vile Leseni ya biashara, hati miliki; hufanywa kwa mfumo wa wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS)
Hatua za lazima za kuingia kwenye mfumo wa ORS ni kama zifutazo;

(i) Kuwa na namba ya Utambulisho wa Utaifa inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Namba ya Utambulisho wa Utaifa ndiyo kitambulisho pekee cha kuingia kwenye mfumo wa ORS. Wakurugenzi na Makatibu wa Kampuni pamoja na Namba ya Utambulisho wa Utaifa ni lazima pia wawe na Namba ya utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na kama siyo watanzania wanapaswa kuwa na namba ya pasi ya kusafiria.

Kama ni mgeni (siyo Mtanzania) ambaye anatarajia kusajili Kampuni Tanzania anatakiwa awe na namba ya pasi ya kusafiria (Passport Number) au namba ya kitambulisho cha utaifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

(ii) Wakati unaandaa Malengo na Katiba ya Kampuni (Memorandum and Article of Association) hakikisha malengo unayojiwekea yameendana na shughuli unazozichagua kwenye mfumo wa ORS kwa mujibu wa ‘ISIC classification’ ambayo inapatikana kwenye mtandao na kwenye Tovuti ya BRELA www.brela.go.tz

Ili kuepuka usumbufu na kuchelewa hakikisha unakuwa na namba ya utambulisho wa Utaifa pamoja na namba ya utambulisho wa mlipa kodi kabla ya kuanza taratibu za usajili. Kwa kampuni zilizosajili zilizowasilisha maombi ya kusajiliwa kabla ya tarehe 1 Februari 2018, tafadhali zingatia yafuatayo:-

(i) Kuwa na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (National Identification Number (NIN) inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

(ii) Wakurugenzi na Katibu wa kampuni kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (NIN), kwa wasio Watanzania wawe na namba ya pasi ya kusafiria.

(iii) Ingia kwenye mfumo na uchague ‘Filing Annual Returns/ Accounts ingiza taarifa muhimu.

(iv) Kuhakiki taarifa za kampuni yako katika ofisi ya Msajili wa Makampuni ikiwa nyaraka kwenye jalada lako hazijasajiliwa au hujawasilisha Mizania (annual returns) ya miaka ya nyuma.

Note:Bila kuweka nyaraka zako kwenye mfumo, hutaweza kuwasilisha taarifa/mizania ya Mwaka, kubadilisha Makatibu wa kampuni, taarifa za benki na kadhalika.