• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Wanachuo

Verified ✓
Staff member
#1
Kuna vijimisemo vifupi vimeibuka huku kwenye mitandao kwa sasa, yaani ni burudani tupu.

Ukivisoma mwisho lazima ubaki mdomo wazi au ucheke, baadhi ya niliyokutana nayo naweka hapa, pia karibuni kwa wenye zaidi tuburudike pamoja.
Tuanze na hivi:-

1. Leo kidogo nipigwe na mwanamke baada ya lifti kusimama, wakati tupo kwenye lifti Nilikua nayaangalia maziwa yake akasema "Bonyeza moja" mimi si nikalibonyeza yaani hadi sasa bado najiuuliza nilipokosea?

2.Hivi utajisikieje utakaposikia rafiki yako wa karibu hajaja kwenye mazishi yako? Nadhani mimi sitamwongelesha tena!
nafikiri nakaribia kupona

3.Nimenunua chips ili nile. Kwa bahati mbaya mtoto wa mama mwingine amekaa karibu na mimi akaanza kuzililia. Imebidi nivae earphones. Napenda watoto, ila utoto ndio sipendi.

4.Jana nimepita njia ya mkato makaburini, warembo wawili wakawa wananikimbilia wanatetemeka eti tunaogopa kupita peke yetu na mimi nikawajibu hata mimi nilivyokuwa hai nilikuwa naogopa sana. Wakazimia.

Sipendagi kufatwa fatwa.