• Mpendwa, Wizara inapenda kuelekeza shule zote za Msingi na Sekondari zitakazofunguliwa kuanzia tarehe 29/06/2020 kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote kuhusu kujikinga na Virusi vya Corona.

Kauli ya Jaji Kaijage na yanayopangwa kufanywa na NEC kwa wagombea Urais

#1
Kauli iliyotolewa jana na Jaji Kaijage ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kuvitaka vyama kuteua Wagombea makini ili baadaye Tume isilaumiwe siyo ya bahati mbaya.

Taarifa za uhakika nilizopata toka ndani ya NEC ni kuwaengua Lissu na Membe kwa technicalities. CHADEMA NA ACT Wazalendo waangalie hizo technicalities mapema wajiandae kisaikolojia.

Uongozi wa juu uliopo hautaki kabisa kampeni hasa kwenye nafasi ya juu ya uongozi. Wangependa kubaki na akina shibuda na lipumba ili kampeni zisiwe na msisimko.

Lissu ana hoja ya maadili ya kuvuliwa ubunge, Nyalandu na Membe wana hoja za kufukuzwa uanachama wa chama chao. Wanasheria wanahaha kutafsiri hoja hizo katika misingi ya kikatiba ili kuwaengua ulingoni na malaika mkuu apite kimya.

Tahadhari kubwa ifanyike na sauti zipazwe.