• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Kilimo bora cha Mananasi: Uandaaji wa shamba, upandaji, utunzaji wa mimea na uvunaji wa mananasi

#1
Jana niliwasilisha mkusanyiko wa mada zinazohusu ufugaji wa kuku..

Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:

Ardhi
 1. Ardhi ya kilimo
 2. Shamba kwa ajili ya kilimo Shamba kwa ajili ya kilimo
 3. Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga
 4. Ardhi kwa Kilimo cha Kitunguu Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko
Mazao
 1. Mazao gani yanafaa kwa kilimo Chalinze? Part 1 Mazao gani yanafaa kwa kilimo Chalinze?
 2. Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya Chalinze? Part 2 Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya Chalinze?
 3. Kilimo cha Mitiki: Utaalamu Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
Mikakati katika kilimo
 1. kilimo-wakulima wa Jf getting together
 2. Kilimo kwanza initiative
 3. Power tiller na dhana ya kilimo kwanza
 4. Kwanza Kilimo?l
 5. Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo
Haya ndio nimeweza kukusanya kwa leo.. hopefully hii itasaidia kutoa mwanga kwa wale wanaotaka kuperuzi posts mbalimbali.

tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.

Gharama zitakuwa hivi:
 1. Ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
 2. Utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
 3. Gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
 4. Mbolea 100,000.
 5. Matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
 6. Jumla 1,500,000/-
Mapato
Nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

Faida :
Ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

Soko likoje
Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). Nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-

Mfano hai
Kamuulize ndugu Eric Shigongo mambo anayofanya Kiwangwa na anapata nini?-

Mwenye taarifa zaidi au anayetaka kukosoa ni vema amwage hapa.

==========
Nanasi ni tunda la kitropiki, linalopendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma.

Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.

Hali ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.

Udongo unaofaa kwa kilimo cha nanasi
Kwa kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.

Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa (flat-bed) au kwa matuta (furrows).

Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.

Upandaji wa mananasi
Mara nyingi wakulima waliowengi hutumia kikonyo aina ya Crowns kupanda zao hili. Crowns ni majani yaliyoota juu ya tunda la nanasi. Uzuri wa kikonyo hiki, mkulima au mtu wa kawaida anaweza kuvikusanya baada ya kununua tunda la nanasi sokoni au baada ya kula tunda la nanasi, ni tofauti na aina nyingine za vikonyo kama Slips na Suckers ambavyo mpaka vipatikane shambani.

Zao la nanasi hupandwa kwa nafasi, nafasi inayotakiwa ni kama ifuatavyo; Shina hadi shina sm 30 na mstari hadi mstari sm 60, pia unaweza ukapanda kwa kuacha sm 120 kila baada ya mistari miwili (inayoachana kwa sm 60). Kwa nafasi hii kutakua na wastani wa mimea 36,350 kwa Hekta moja.

Hatua kwa hatua namna ya kupanda
 • Kata kikonyo chako kilichopo juu ya tunda la nanasi (Crowns), ondoa sehemu ya tunda iliyobakia kwenye kikonyo kwani huwa na sukari nyingi.
 • Acha vikonyo vyako vikauke ndani ya chumba chenye giza kwa muda wa wiki 1 hadi 2. Unapovipanga hakikisha unavigeuza juu chini, sehemu iliyokatwa iangalie juu.
 • Baada ya kukauka lowanisha vikonyo vyako kwenye dawa ya ukungu na dawa ya wadudu.
 • Panda vikonyo vyako kwa nafasi ya sm 30 shina hadi shina na sm 60 mstari hadi mstari, vikonyo hivyo vizame ardhini kina cha sm 3, pia unaweza ukachimba mashimo yenye kina cha sm 7 au 10. Baada ya hapo shindilia udongo kiasi.
 • Mwagilia maji kama udongo ni mkavu ili kuharakisha kikonyo kutoa mizizi.
 • Itachukua muda wa miezi 15 hadi 24 kuvuna nanasi.
Kuweka mbolea
Zao la nanasi huitaji mbolea hususani kirutubisho cha nitrojeni, baada ya kikonyo cha nanasi kutoa machipukizi, weka mbolea jamii ya NPK juu ya ardhi karibia na shina la nanasi.

Kirutubisho cha Nitrojeni hufaa sana kuongeza ukubwa wa matunda na mavuno kwa ujumla, Pia ni vyema ukatumia mbolea za asili pamoja na za kisasa. Kiasi cha mbolea za asili kinachohitajika kwa Hekta moja ni Tani 5 hadi 10. Pia kirutubisho cha Phosphate (P) huitajika ili kuboresha mizizi na kuongeza uzalishaji, hivyo mbolea jamii ya NPK hufaa sana kwa zao hili.

Pia mbolea za kwenye majani (Foliar fertilizer) hufaa sana kwa zao hili, Ingawaje kirutubisho cha Nitrojeni (N) kikizidi sana husababisha matunda ya nanasi kuwa na maji mengi kuliko utamu.

Pia kirutubisho cha Potassium (K) hufaa sana kwani husaidia matunda kukomaa mapema na kua bora sana. Tumia mbolea jamii ya NPK ili kuupa mmea kirutubisho cha Potassium (K).

Palizi (Weeding)
Hakikisha shamba lako linakua safi wakati wote kwa kuondoa magugu shambani aidha kwa kutumia jembe la mkono au kwa kutumia madawa ya kuua magugu (Herbicides). Njia hii ya kutumia kemikali za kuua magugu hufaa sana kipindi cha awali cha uandaaji shamba, yaani kabla ya kupanda, kwa sababu lazima tuwe na tahadhari ya kiafya ili tupate matunda ya nanasi yasiokua/yaliyo na kiasi kidogo cha masalia ya kemikali (Pesticides residue)

Kuondoa magugu shambani hasaidia kupunguza kiwango cha wadudu waharibifu na magonjwa, kwani magugu hayo ndio makazi ya wadudu waharibifu na chanzo cha vimelea vya magonjwa mbalimbali ya mmea.

Wadudu waharibifu na magonjwa

A: Wadudu waharibifu

1. Nematodes/Minyoo Fundo (Meloidogyne javanica and Pratylenchus brachyurus)

Minyoo hawa husababisha mizizi kuwa na vinundu na mara nyingine madoa madoa hatimae mizizi huoza na kufa baadae mmea hunyauka na kufa.

Namna ya Kudhibiti
 • Uwe na tabia ya kubadirisha mazao
 • Hakikisha shamba lako linakua safi wakati wote
 • Kama utaweza tumia mazao yoyote ya mti wa mwarobaini (kama Unga uliosagwa kutokana na majani, matawi au magome ya mwarobaini) kwa kuweka kwenye udongo.
2. Pineapple mealybug (Dysmicoccus brevipes)Hawa ni wadudu wenye umbile kama yai, wana rangi ya pinki, wanakua na urefu hadi mm 3 na wanatengeneza unato mweupe kwenye mwili wake wote. Mdudu huyu ni hatari sana kwa uzalishaji wa nanasi kwani husambaza ugonjwa wa virusi wa nanasi uitwao "Mealybug or Pineapple Wilt Virus" (Ugonjwa wa mnyauko).Wadudu hawa mara nyingi huwa kwenye mizizi ya nanasi na huzaliana sana kwenye shina la nanasi. Baada ya kuzaliana sana kwenye shina la nanasi, baadae huenea kwenye maua, matunda madogo na matunda yaliyokomaa, pia hufika kwenye majani ya juu ya tunda la nanasi (Crown leaves)

Athari
 • Wakiwa kwenye majani husababisha rangi ya njano kuanzia mwishoni mwa jani (leaf tips), baadae njano hiyo husambaa hadi jani zima na hatimae majani hukauka.
 • Wakila maua husababisha majeraha ambayo mara nyingine hukumbana na chavua (Spores) ambazo zina ugonjwa wa ukungu (Fungal disease), hatimae husababisha ulemavu unaoitwa 'Black Spot'
 • Wakila mizizi husababisha mizizi kuoza na baadae mmea kunyauka.
Wadudu hawa (Mealybugs) huishi salama kwenye maeneo yao na kuongezeka kwa sababu huishi pamoja na jamii mbalimbali ya sisimizi (Ants). Sisimizi hawa, hususani sisimizi wenye kichwa kikubwa (Pheidole megacephala) hawamdhuru mealybug bali hula unato kama asali unaotoka kwenye mwili wa mealybug, hali hii husaidia kuwapunguzia utando huo ambao ukizidi kwa mealybug wadogo husababisha mwili wa mealybug kukakamaa.

Sisimizi hawa (Ants) wanapokua wanakula unato wa mealybugs (Honeydew), huwabugudhi wadudu wengine wanaokula mealybugs (Natural enemies), kwa hiyo mealybugs hupona kuliwa kwa sababu ya uwepo wa sisimizi hao (Ants). Vilevile sisimizi hawa huwasambaza mealybug kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kuwabeba kwenye midomo yao.

Namna ya kudhibiti
Tumia dawa mbalimbali za wadudu zinazoweza kuwaangamiza hao sisimizi (Ants), wakishaangamia mealybug wanakosa ulinzi hivyo huangamizwa kirahisi na wadudu wengine (Natural enemies).

Njia nyingine ni kutibu vipandikizi au vikonyo hususani Crowns kwa kutumia maji ya moto yenye nyuzi joto 50°C kwa dakika 30 (Loweka vikonyo hivyo kwenye maji hayo ya moto kwa dakika 30).

Njia hii husaidia kuondoa mazalia ya melybug na kusaidia mmea utakaoota kutokua na wadudu hawa pia kutokuwepo kwa uwezekano wa mmea kupata ugonjwa wa mnyauko "Mealybug / Pineapple Wilt Virus" unaosababishwa na virusi vinavyosambazwa na wadudu hawa.

Uvunaji wa nanasi
Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva. Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa sawa.

Kwa wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa wakaii mmoja, angalau 80% ya mimea yote.

Vuna wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu. Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.

Utunzaji wa nanasi
Hifadhi nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo chake kikielekea juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3 baada ya kuvuna ili kutunza ubora wake.