• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

King98: Natamani Busti ya Mondi Kupata Mashabiki Bongo

#1

Msanii wa Zimbabwe, Ngonidzashe Dondo (22) ambaye ni maarufu kama King98
MSANII wa Zimbabwe, Ngonidzashe Dondo (22) ambaye ni maarufu kama King98, ametua nchini hivi karibuni kufanya ziara fupi kwa lengo la kuutambulisha wimbo wake wa ‘Kachiri’ ambao alimshirikisha msanii mahiri nchini wa Bongo Fleva; Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.

AMANI limefanya mazungumzo maalumu na msanii huyo, ambaye amefunguka mambo mbalimbali juu ya matamanio yake kukua kimuziki na kuteka pia soko la Bongo.
AMANI: Ilikuaje ukakutana na Diamond na kufanya naye kazi?

KING98: Nilikutana na Diamond kupitia Davido (msanii kutoka Nigeria) yeye ndiye aliniunganisha naye.AMANI: Ni jambo gani kubwa lililokuleta Tanzania?

KING98: Nimekuja kufanya kazi na S2kizzy, ambayo ni kutoa album yangu mpya maana ujio wangu wa kwanza sikupata muda wa kuzunguka kwenye media mbalimbali kwa sababu nilikuja kwa dhumuni moja tu, kufanya kazi na Diamond kwa muda wa siku mbili.

AMANI: Ulianza lini kazi ya muziki?

KING98: Nilianza nikiwa na umri wa miaka 13, bado nilikuwa shule.

AMANI: Kwanini aliamua kuja kufanya kazi na Diamond Platnumz na si wasanii wengine?
KING98: Kwa kuwa nyimbo zake zimewika maeneo mengi ndani na nje ya Afrika, kama Nigeria na Afrika ya Kusini. Hilo ni mojawapo ya jambo lililopelekea kupata motisha ya kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka Afrika Mashariki kama Diamond Platnumz. Ninaamini kolabo yangu itafanya poa na kusikilizwa zaidi Afrika Mashariki.

AMANI: Je, ulitozwa kiasi chochote cha fedha kufanya kazi na Diamond Platnumz?
KING98: Kuhusu suala ya malipo siwezi kulizungumzia kwa sababu lipo chini ya uongozi wangu.AMANI: Nini maoni yako baada ya kufanya kazi na Diamond?
KING98: Namshukuru Diamond kwa sababu yeye ndiye sababu wimbo kuwa maarufu na kujulikana sana.AMANI: Mbali na kufanya kazi na S2kizzy, ni producer gani mwingine ungependa kufanya naye kazi?KING98: Ningependa kufanya kazi na Laizer.

AMANI: Unatamani kufanya kazi na msanii gani wa kike hapa Tanzania?
KING98: Nitamani kufanya kazi na Zuchu, Rosa Ree au Vanessa Mdee, lakini yupo mbali kwa sasa.
AMANI: Ni wasanii gani wengine mbali na Diamond, umefanya nao kazi Tanzania?

KING98: Nimefanya kazi na Rayvanny, Jux na Younglunya.
AMANI: Unajiona wapi miaka miwili ijayo?

KING98: Ndani ya miaka miwili ijayo najiona msanii mkubwa nikifanya matamasha na wasanii wakubwa kama Chris Brown wa Marekani na kuwa na maendeleo makubwa kwa sababu ninatimu kubwa inayoshirikiana nami.

AMANI: Ulianza muziki katika umri mdogo, familia yako ilichukuliaje suala hilo?

KING98: Kwa mara ya kwanza, wazazi wangu hawakukubaliana na wazo langu hadi nilipopanda kwenye jukwaa wakati Casper Nyovest akitumbuiza, ambapo alinipa nafasi ya kuimba na kusema ninakipaji. Jambo hilo likawashawishi familia yangu.

AMANI: Ungependa mashabiki zako wakujue wewe ni mtu wa aina gani?KING98: Mimi ni mpole, muelewa, siku zote niko tayari kujifunza na pia ni mtu wa watu.

AMANI: Je, umeoa au upo kwenye mahusiano?

KING98: Nina mchumba yupo Zimbabwe kwa sasa sababu ya likizo ya Corona, lakini bado ni mwanafunzi anayesoma Afrika Kusini.

AMANI: Una neno gani kwa mashabiki zako kutoka Tanzania?
KING98: Ninawashukuru kwa mapokezi mazuri ya kazi yangu na wategemee mambo mazuri kutoka kwangu.
AMANI: Asante sana King98 kwa muda wako.
KING98: Asanteni pia