• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Mapenzi ya dhati katika historia

#1
Suala hili limekuwa likijadiliwa kwa muda mrefu. Kwa hakika mapenzi ni adhabu ambayo mtu hajitambui anapojipa adhabu hiyo. Hata kuna msemo unaosema, “Laiti mapenzi yangekuwa ni hiari, basi ningekuwa mwalimu wa kutopenda.”

Je, unadhani unadhani mfalme Salim Şah alitaka kumpenda Anarkali ambaye alikuwa mnenguaji kwa wakati huo?
Muziki

Kulinga na kisa hicho, mfalme Salim Şah, alimuona Anarkali katika tamasha moja ya burudani iliyofanyika ndani ya kasri. Mfalme Salim Şah akavutiwa mno na Anarkali aliyekuwa akicheza katikati ya wanawake wengine.

Anarkali alicheza kwa maringo na kufanya harakati za kuvutia kama vile kujishika nywele zilizomuongezea uzuri na urembo wa muonekano wake.

Anarkali alicheza kwa huku akizunguka na hatimaye akajipata ana kwa ana na mfalme Salim Şah aliyeuteka moyo wake.

Siku zilizidi kuyoyoma na mfalme Salim Şah akazidi kumuwaza mrembo huyo aliyekuwa tayari kumpa moyo wake. Bila shaka mapenzi ni hisia zinazoongezeka na muda.

Mfalme Salim Şah alikuwa akipoteza muda wake mwingi kumfuata binti huyo ili amtazame anavyocheza. Hatimaye mfalme Salim Şah akashindwa kuvumilia na kuamua kufunga ndoa na binti huyo. Hata hivyo, kwa mujibu wa tamaduni za jamii, sheria hazikumruhusu mfalme kufunga ndoa na msichana wa kawaida asiyekuwa na hadhi yoyote katika utawala.

Mfalme Salim Şah, akaamua kuwasilisha ombi la kutaka kumuoa Anarkali kwa babake Han Akbar huku akiwa na matumaini ya kukubaliwa. Lakini babake akaona ombi hilo kutokuwa na maana yoyote na kulikataa.

Wakati huo huo, babake akamwekea mwanawe mfalme Salim Şah marufuku ya kumuona tena binti yule.

Licha ya hayo yote, mfalme Salim Şah hakukata tamaa kutokana na mapenzi yaliyozidi kuongezeka moyoni mwake.

Baada ya muda mrefu, taarifa za mapenzi ya mfalme Salim Şah aliyokuwa nayo kwa Anarkali zikaanza kuenea kwa viongozi wote. Kwa bahati nzuri, binti huyo pia alikuwa amependa mfalme Salim Şah ingawa hakusema wala kudhihirisha mapenzi yake.

Wapenzi hao wawili wa siri walikuwa wakikutana kila walipopta fursa ya kuonana. Watu wote walikuwa wakiona mapenzi yao kuwa ya bahati mbaya.

Kila taarifa zilipokuwa zikienea kuhusu mapenzi ya Anarkali mfalme Salim Şah miongoni mwa wakazi, babake Han Akbar alikuwa akikwera sana. Alikuwa akimuita mwanawe na kumfokea kwa vitisho ili amuache binti yule.

Lakini mapenzi yao hayakuweza kuzuiwa kwa kitu chochote kilichowekwa mbele yao.

Mfalme Salim Şah aliendeleza juhudi zake za kuonana na Anarkali kila mara na taarifa za mapenzi yao zikazidi kuenea kila mahali. Kutokana na kero alilokuwa akilipata babake Salim Şah kwa habari za mwanawe kuendelea kumpenda Akbar Han, akaamua kutafuta suluhisho mwenyewe.

Akbar Han aliamua kujenga chumba kilichozungukwa n anne ndefu zisizokuwa na madirisha katikati mwa mji. Kisha akaamuru askari kumkamata Anarkali na kumfungia katika chumba hicho kilichokuwa na mlango mmoja pekee.

Lengo lilikuwa ni kumzuia kuonana na mwanawe na kuangamiza mapenzi yao.
Mfalme Salim Şah akaanza kutafuta sehemu aliyofichwa Anarkali hadi akaipata na kujaribu kuvunja ili kuingia na kumfungulia. Alilia mno kwa ajili ya kutaka kumuokoa mpenzi wake.

Lakini hakuweza kubomoa wala kufungua chumba hicho kwa kuwa kilijengwa kwa kuta imara zisizoweza kubomoka. Mfalme Salim Şah akabaki akilia kwa uchungu pasi na kufanya chochote.

Salim Şah kumwambia babake Akbar Han, kuwa amekata tamaa na mapenzi hayo, hakumuonea huruma Anarkali.

Badala yake, aliendelea kumfungia Anarkali kwa siku nyingi hadi kufikia hatua ya kudhania kwamba Anarkali hangeweza kutoka salama salmini kwenye chumba hicho.

Hakuna aliyeonekana mbele ya chumba hicho alichofungiwa Anarkali ispokuwa Salim Şah pekee aliyekuwa anaumia ndani kwa ndani kwa maumivu na machungu ya mpenziwe.

Misimu ya kiangazi na baridi kali ilikuja na kuondoka lakini Salim Şah alibakia pale pale akiomboleza kwa kumpoteza Anarkali.

Ghafla akasikia harakati kutoka ndani kuta za chumba kile.

Baadaye kidogo kuta zikaanza kutoka nyufa na kubomoka. Salim Şah akaanza kufuatilia njia iliyoelekea ndani ya chumba kile na watu wakakusanyika tena kutazama kilichokuwa kikitokea.

Watu waliokusanyika wakamsaidia Salim Şah kuondoa mabaki ya mawe ya kuta zilizobomoka kana kwamba walikuwa na matumaini ya kumuona Anarkali akiwa hai tena.

Asubuhi iliyofuatia, watu wakaona ndani ya kuta zile maua ya waridi ya rangi nyekundu yaliyotapakaa. Maua yaliyochanua kwa wakati mmoja na kupendeza kama Anarkali.

Wakati huo huo, Salim Şah akavutiwa mno na maua yale ya waridi kiasi cha kumuondoa maumivu ya moyo aliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

Salim Şah aliyesubiria kwa miezi mingi nje ya chumba kile alichofungiwa Anarkali, hatimaye alikuwa na furaha baada ya kuona maua yale ya waridi yaliyomsisimua na kuamsha hisia zake za mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa mpenziwe Anarkali.

Alikuwa ni kama aliyemuona tena mpenziwe.

Watu walioshuhudia tukio hilo la Salim Şah na kifo cha mpenziwe, walifafanua uchungu wa mapenzi yaliyokuwepo kati ya wapenzi hao wawili kujieleza kupitia maua ya waridi. Wanasema kwamba maua ya waridi mekundu ni ishara iliyodhihirisha kwamba moyo wa Anarkali uliojaa mapenzi ya dhati.

Kwa mtazamo wao, wanasema kwamba Anarkali aliegemea kuta za chumba kile kwa lengo la kumuonyesha mpenziwe jinsi alivyompenda kwa dhati na kufanikiwa kufanya hivyo kwa ishara ya maua.

Mmoja wa washairi waliosikiliza kisa hiki cha kusikitisha Feyzi Halıcı alitunga shairi moja zuri linaloleta kumbukumbu kwa wapenzi wengine.