• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

MBINU ZA KUJIFUNZA ENGLISH KWA URAHISI NA HARAKA

Edgar Mbele

Moderator
Staff member
#1
Kwa uzoefu wangu wa kujifunza na kuweza kutumia lugha nne tofauti yaani Spanish, English, Zulu na Xhosa nimejifunza kuwa kuna mambo ambayo yanarahisisha sana namna ya kujifunza lugha. Hivi karibuni nilitumia mbinu hizo kujifunza lugha ya Spanish kwa miezi mitano tuu.
Pia kama mwalimu binafsi wa lugha ya nimeona wanafunzi wangu wengi wakikwama kupiga hatua katika kujifunza English kwa namna isiyo sahihi ya jinsi ya kujifunza wanayojaribu kufanya. Ndio maana nimeamua kuandika makala hii kama muongozo kwa wanafunzi wangu wa English lakini pia kushare na jamii kwa ujumla.
Ni ukweli usiopingika kuwa kabla ya kujifunza kitu chochote ikiwemo kujifunza lugha ni muhimu kujua namna ya kujifunza kitu husika, ili uweze kujifunza kwa ufanisi na kwa urahisi.
Hata hivyo elewa kuwa ninaposema kujifunza kwa urahisi, simaanishi kuwa basi kujifunza kwako hakutakuwa kugumu.
Baadhi ya mambo katika lugha yatakuwa magumu hata hivyo kwa mbinu sahihi na kwa bidii ya dhati, mchakato wako wa kujifunza utakuwa rahisi zaidi kuliko bila kuwa na mbinu na ufahamu wa namna sahihi ya kujifunza.
Hii ni sehemu ya kwanza ya makala hii .
Vifuatavyo ni vipengele vya hizo mbinu za kujifunza lugha hususani lugha ya English.
1. Kudhamiria kuweza:
Usianze au kuendelea kujifunza kiingereza bila kujiaminisha na kudhamiria kuweza haswa kwa ufasaha. Haitoshi tuu kutamani kuweza kiingereza, unahitaji nguvu ya dhamira ya toka moyoni , na kujiaminisha kuwa wewe unaweza.
2. Kujiwekea muda maalum wa kufikia kiwango fulani :
Haitoshi tuu kudhamiria kuweza kuongea lugha ya kiingereza. Unahitaji kujiwekea malengo na mikakati ya kufikia hilo lengo na iwe kufikia lengo fulani ndani ya muda maalum.
Njia bora ya kujiwekea muda ni kuligawa lengo lako la kufahamu lugha katika vipengele vidogo vidogo halafu unaweka malengo ya kufanikisha hivyo vipingele vidogo vidogo ndani ya muda fulani.
Kwanza fahamu picha kubwa ya yote unayotakiwa kujifunza, kisha jiulize yapi kati ya hayo tayari unayajua au pengine una ‘idea’ nayo.
Hivyo weka malengo kwa kila kipengele kuendana na uwezo wako wa kuelewa.
Mfano ukishajua vipengele vyote mfano vya TENSES, jiulize ndani ya muda gani utaweza kukamilisha tenses. Hivyo hivyo kwa vipengele vingine .
Kutambua viungo mbalimbali vinavyounda sentensi:
Kila unachoandika, kuongea, kusikia au kusoma ni SENTENSI. Katika sentensi unaandika, kusoma, kusikiliza au kuongea maneno. Hata hivyo ili kurahisisha watu kujifunza lugha, maneno hayo yamegawanywa katika makundi , na hayo makundi yanafafanua matumizi na kanuni kuhusu kila neno katika kundi husika.
Mfano sentensi hii : Will you come to school ? - Je utakuja shule ?
Hapa tuna maneno matano, na yanatoka katika makundi yafuatayo:
Verbs: Will na Come
Pronoun: You
Proposition: TO
Noun: School
Kufahamu kanuni zinazoongeza makundi haya zitakafunya ujue kwanini hayo maneno yamepangiliwa hivyo yalivyo , mfano kwanini haikuwa COME WILL TO SCHOOL YOU ?
Katika kujifunza kanuni hizi ndipo utakapojitofautisha wewe na wale ambao wanadhani kujifunza lugha ni kujua maneno mengi.
Kuna watu wengi wanajua maneno mengi ya kiingereza na ni wepesi wa kuchanganya kiswahili na kiingereza wakati wa mazungumzo ila inapofika kuongeza kiingereza tuu kwa mfululizo inakuwa ni tabu kwakuwa hawana ujuzi wa kuunda vema sentensi.
3.Kusoma kwa mpangilio:
Baada ya kufahamu kuwa lugha ina vipengele kadhaa vinavyounda sentensi na kanuni zinazoongoza kila aina ya maneno , bila kusahau nyakati –tenses, jiwekee utaratibu wa kusoma hatua kwa hatua kwani vipengele vingi vinaendana.
Mfano kama haujaelewa vizuri tenses, itakupa shida kuelewa active and passive voice, na reported speeches.
4. Kusoma kwa mfululizo bila kukatisha:
Mbinu nyingine ni kuhakikisha kuwa unajifunza lugha kwa muda maalum na kwa mfululizo. Sio unajifunza kwa "manati" mara moja au mbili tuu ndani ya mwezi.
Ili kufanikiwa kujifunza kwa urahisi na kwa haraka hakikisha unatenga muda walau mara tatu kwa wiki, na kwa muda wa walau masaa mawili kila siku na hakikisha unasoma hivi kwa muda mrefu mfano walau kwa miezi mitatu mfululizo kwa kasi hiyo hiyo ya kujifunza.
Kwanini unahitaji kujifunza kwa mfulululizo ? Ni kwa sababu kujifunza lugha kunahitaji sana kukumbuka na kuhusanisha uelewa wa vipengele tofauti vya lugha.
Hivyo kujifunza mfululizo kunatuma ujumbe kwa ubongo wako kuwa hayo unayojaribu kuhifadhi katika kumbukumbu yako ni ya muhimu, hivyo nao unatenga nafasi ya kukusaidia kuyapata haraka unapohitaji –yaani kumbukumbu ya haraka.
Kumbuka pia hata kama unasoma na yanakua magumu, ukiendelea kurudia mara kwa mara jambo lile lile baada ya muda unajikuta umeshajenga aina fulani ya kumbukumbu na uwezo wa kuhusanisha yale uliyojifunza zamani na taarifa mpya ya jambo hilo hilo husika.
5. Kufahamu matumizi ya nyakati na kanuni zake :

Mbinu hii inahusu vitu viwili muhimu sana, kwanza kujua uwepo wa nyakati na matumizi yake yaani je katika hali ipi unatumia present tense, au past tense, au future tense, halafu kitu kingine cha pili cha muhimu sana ni kujua kanuni zinazoongoka namna ya utungaji wa sentensi katika kila aina ya nyakati.
Hitimisho:
Hii ilikuwa sehemu ya kwanza ya makala hii ya mbinu za kujifunza kwa haraka na kwa urahisi lugha ya kiingereza. Usikose kusoma sehemu ya pili.
Kwa ujumla wake makala hii imekuonyesha kuwa kujifunza English ni zaidi ya kusikiliza, na kusoma , unahitajika wewe mwenyewe kuingia hasa katika mchakato wa kuelimika kwa kufanya bidii kujikumbusha na kurahisha namnaya kuelewa unachosoma