• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

MICHO AWATAKA CHAMA NA CHIRWA

#1
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zambia Milutin Sredojevic “Micho” amewakata katika kikosi cha Taifa Wachezaji Clotous Chama wa Simba na Obrey Chirwa wa Azam FC kwa kudai wameonesha utovu wa nidhamu kwa kushindwa kuungana na wenzao kama walivyotakiwa.

“Tulitarajia Wachezaji wawili kutokea Tanzania ambao walitakiwa kusafiri Jumatatu usiku, hata hivyo waliachwa na ndege na sasa wanaomba waje kesho yake, hiyo sio sawa wakati kuna mchezaji mmoja ambaye amewasifiri Kilometa elfu 10 kutokea Urusi yuko hapa na wao wako nchi jirani tu hapo sio sawa” — Micho

“Utovu huo wa nidhamu sitaruhusu kwa yoyote kuwa mkubwa kuliko nchi, nimeamua kuwaondoa katika mchezo huu hadi taarifa zaidi zitakopotolewa wakati mwingine”