• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

MISINGI YA UFUNDISHAJI VITENDO VYA MASOMO YA ELIMU YA AWALI

Edgar Mbele

Moderator
Staff member
#1
kids-pic3.jpg


Kwa ujumla katika utoaji wa e/a kuna vitendo sita vya masomo

1.Vitendo vya hesabu
2.Vitendo vya lugha ya kiswahili
3.English L/A
4.Vitendo vya sayansi
5.Vitendo vya haiba na michezo
6. Vitendo vya sanaa
Kuna misingi sita muhimu ya kuzingatia
1.Ufundishaji na ujifunzaji wa E/A unafanyika kwa vitendo. Kwa nini tunafundisha E/A kwa vitendo? Kumjengea mtoto uwezo wa kuweka kumbukumbu ya kudumu, kuelewa kwa haraka, kuhusianisha vitu,
-Kuruhusu mtoto kutumia milango mingi ya fahamu n.k
-Anakuza ari ya kujifunza
-Kujenga ushirikiano miongoni mwa watoto
-Anakuza uwezo wake wa lugha (misamiati mbalimbali)
 1. Ukuaji na ujifunzaji vinahusiana. Kujifunza kwa mtoto lazima kutegemee ukuaji
 2. Kila mtoto anajifunza kulingana na uwezo wake. Uwezo wa kiakili, kimwili na kimaono. Watoto wanatakiwa wawe wametawanyika kutokana na uwezo wao na tofauti zao
 3. Maendeleo ya mtoto na ujifunzaji vinategemeana ushirikiano wa mwalimu, mzazi, familia au jamii inayomzunguka
-Mzazi (lishe, afya, malezi bora, mavazi, motisha, ulinzi na usalama, vifaa stahiki, upendo
-Mwalimu (upendo, mazingira, maadili, vifaa, ulinzi na usalama, zana/vifaa vya ujifunzaji
 1. Mtoto anajifunza kutokana na maarifa ya awali aliyo nayo na jinsi anavyojihusisha na mazingira. 1. maarifa ya awali 2. Mazingira stahiki (darasa, zana, usafi, utulivu, hewa
 2. Kuzingatia usafi na usalama wa mtoto na mazingira ya kufundishia na kujifunza
 3. Mbinu za kufundishia vitendo na ni katika masomo yote
 4. Zana ya kufundishia, kuandaa zana stahiki mfano: vitendo vya kiswahili kusalimia
 5. Kujitambua kwa kukabiliana na hasira, sauti ya kawaida
Misingi ya kufundisha vitendo vya lugh ya kiswahili
1.Kufundisha stadi za kusikiliza na kuzungumza kwanza (principles of listening and speaking)
2.Kufundisha tadi za kusoma
3.Kufundisha stadi za kuandika
Misingi ya haiba na michezo
1.Kujenga tabia ya ushirikiano, uvumilivu na kuheshimiana
2.Kujua haki za mtoto na kutimiza wajibu wake
3.Kukuza stadi mbalimbali za michezo na kujenga afya njema kwa mtoto.
Misingi hii inachangia sana katika kujifunza kwa mtoto kwa haraka kuliko vitendo vingine kama vya kuhesabu, sayansi n.k.
Swali:
Jadili ni kwa nini uwezo wa watoto katika kujifunza unatofautiana na eleza utawasaidiaje watoto wenye uwezo tofauti wa kujifunza katika Elimu ya Awali.
MBINU ZA KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA
 • Njia shirikishi
 • Njia zisizo shirikishi
 • Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya Mbinu za kufundishia na Zana za kufundishia
MBINU
 • Nyimbo
 • Michezo
 • Maswali na Majibu
 • Kazi mradi
 • Onesho mbinu
 • Igizo dhima
 • Majadiliano
 • Hadithi
 • Ziara
 • Majaribio/ inquiry
 • Bungua-Bongo
 • Mihadhara
 • Kualika mgeni
 • Kisa mafunzo
Zipo mbinu zaidi ya zilizoorodheshwa hapo juu. Kuna umuhimu wa kufahamu kila mbinu, namna inavyotumika, faida zake na hasara zake. Vilevile kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mbinu za kufundishia na zana za kufundishia. Mwalimu anaweza kutumia mbinu zaidi ya moja katika kufundisha mada moja. zifuatazo ni baadhi ya mbinu cheche za kufundishia watoto wa Elimu ya Awali.
 • Mbinu ya nyimbo
-Wimbo katika vitendo vya hesabu. mfano.,
1, 2, 3, 4, 5,6, 7, 8, 9, 10 tayari
-Naanza kuhesabu namba 1, 2, 3….. . Baada ya kuimba wimbo watoto wanaongozwa kuhesabu
-Chupa mezani
Chupa 1 ongeza moja utapata ngapi? Utapata chupa 2.
 • Tendo la kutoa
Ndege 10 mtini porini wamelala
Wa kwanza akaruka….
Wa pili akaruka
Na wote wakaruka wakaenda juu.
 • Vitendo vya sayansi
Mada ya wanyama
Mee mee mee nalia mee .. Mbuzi na watoto wake analia mee
Moo moo moo nalia moo.. Ng’ombe na watoto wake analia moo
Nyau nyau…..
 • Mada ya mimea
-Maua mazuri yapendezaaa….
Ukiyatazama yana meremetaa
Yaita watoto waje shule
-Maua ya bustani yamechanua x2
Tembelea shule yetu utayaona x2
Maua ya njano utayaona..
zambarao
bluu
 • Vitendo vya haiba na michezo
-Tujioshe mwili mzima twende safi shuleni… x2
Meno tusugue pia nguo tufuee
Nywele tuzichane na kucha tuzikate
– Paulo usije kucheza na sisi una mikono michafu.
 • English Teaching activities
 • Principles of teaching vocabulary items in young children
-Teach vocabulary items that are found within the learners environment
-Use grouping system and not alphabetical system i.e things that are similar like home utensils,
-Never use translation method because translation is a poor method of teaching vocabulary in children
-Do not teach more than one vocabulary item in a single period/ lesson.
 • Other principles
-Oral reading item of writing or speaking good language
-Create a rich environment in classroom
-Never use a cross symbol because it’s a negative environment
-Don’t talk much. Reduce energy of speaking
-Use mixture of different methods in your class integration of skill method.
 • Some of activities in teaching Act of listening
-Listening and tick activities
-Listening and draw
-Listening and color
-Listening and do physical activities
 • Act of speaking
-To mention the name of pupils in class
-Chants – repeat words
-Reading and do activities
-Reading and match
-Reading and match with a picture
-Match sentences to the picture
 • Act of writing
-Match then write
-Coping on blackboard
-Ranking activities
 • Expensive to cheap
-Meal at Hotel
-1kg of sugar
-Cocacola
-Biscuits
-Samosa
 • Big – Small
-Cow
-Sheep
-Goat
-Cock
-Hen
-Cat
 • Mbinu ya Michezo katika matendo ya hesabu
-Mdako
-Snap card
-Kadi za namba mfano
1 ziwe nakala 4
2 ziwe nakala 4
Hadi 9 ziwe nakala 4
Jumla kadi 36
Katika lugha unatumia herufi
a ziwe nakala 4
e ziwe nakala 4
u ziwe nakala 4
 • Domino za nukta
-Mipaka ya namba
Mfano 6
0 + 6 = 6
1 + 5 = 6
2 + 4 = 6
3 + 3 = 6
4 + 2 = 6
5 + 1 = 6
6 + 0 = 6
Nukta zilizopo kwenye kadi zisizidi sita wakati wa kujumlisha. Mfano nukta 4 unaweka nukta 2 ili kupata sita na haipaswi kuzidi.
 • Chati ya namba
 • Yenye vyumba 20
 • Kurusha dadu yenye nukta kisha kufunika namba aliyoipata katika dadu
 • Itamwezesha mtoto kuhesabu kisha kutambua namba na kufunika
Zana za Kufundishia na kujifunzia
 • Kuelezea
– Makundi ya zana
– Aina za zana
 • Maarifa- kufikiri
 • Stadi- ujuzi katika kufanya jambo fulani. Tunahimiza matumizi ya mwili (viugo) katika kufanya kazi
 • Itikadi-utu, kuheshimiana, kushirikiana katika kudumisha utu
 • Mtaala- ni programu ya mafunzo ili mtu aweze kufanya kazi kwa kutumia viungo vya mwili
Dhana ya mitaala
-Nchi yoyote inataka kurithisha maarifa kwa watu wake.
-Ni lazima kushirikiana na wadau mbalimbali kwanza kwa kuangalia falsafa ya nchi, mahitaji ya nchi
-Wataalam mbalimbali, taasisi mbalimbali za kidini na imani mbalimbali
-Mtaala ni utaratibu wa
-Ni jumla ya mipango na uzoefu ulioratibiwa kwa ajili ya mafunzo ya muda maalum
-Mojawapo ya nguzo kuu zitakazotumika ni muhtasari
-Mtaala ni jumla ya mambo yote yanayomwezesha mwanafunzi kupata uzoefu akiwa darasani au nje ya darasa
 • Miataala inaandaliwa na watu wanaoitwa wakuza mitaala kama taasisi ya elimu wakiongozwa na malengo makuu ya elimu yanayotokana na mahitaji ya jamii na falsafa ya elimu
 • Kazi za mtaala
-Kutafuta njia zitakazofikia malengo. Njia, zana
-Kuweka malengo muhimu yaliyokusudiwa
-Unatoa dira, mwongozo wa kumwelekeza mwalimu katika ufundishaji
-Unatoa picha halisi ya falsafa ya nchi
-Mada zinazotakiwa, njia, vifaa na kupendekeza
-Inafafanua matarajio ya jamii. Kukidhi mahitaji ya jamii ili malengo ya mtaala yatekelezeke kwa kuzingatia mila, desturi na
Kwa kurithisha mila za jamii kizazi kimoja hadi kingine
 • Aina za mitaala
-Mitaala rasmi; uliyopangwa mambo yote yaliyoratibiwa. Unaainisha na kuweka mambo yote ambayo mwanafunzi atayapata chini ya uangalizi wa shule na vifaa maalum. Unaonyesha aina mbalimbali za masomo. Utaonyesha njia mbalimbali zitakazotumika na mbinu
-Mitaala isiyo rasmi; mambo yanayofanyika nje ya mtaala uliyo rasmi
 • Ndani ya mtaala tunapata mhutasari, azimio la kazi, nukuu za somo
 • Utekelezaji wa mtaala hutegemea mambo mbalimbali kwa kutumia vifaa mbalimbali kama
-Muhtasari
-Kiongozi cha mwalimu
-Vitabu vya kiada
-Kitabu cha mwalimu
-Maandiko ya rejea
 • Maana ya muhtasari
 • Faida za muhtasari
 • Vifaa vya mitaala viko katika makundi mawili
-Vifaa vya maandishi
-Vifaa visivyo vya maandishi
Dhana ya Azimio la kazi
 • Mpango wa kazi unaoandaliwa na mwalimu kwa kipindi fulani unaomwazesha kufundisha kutoka katika azimio la kazi
 • Mpango wa utekelezaji wa muhtasari wa somo unaotayarishwa kwa kipindi maalum na mwalimu wa somo hausika.
 • Taarifa za awali
– Jina la mwl wa somo
– Jina la shule inayofundishwa
– Mwaka
– Mhula
– Somo
– Darasa
– Mhula
Sehemu ya pili inaonyesha jedwali lenye vipengele 13 baada ya mabadiliko ya mtaala. Sehemu zingine kuna vipengele 11.
Umuhimu wa Azimio la Kazi
1.Linatumika katika kuandaa Andalio la Somo
2.Linamsaidia mwalimu kufundisha mada kwa mtiririko mzuri
3.Linamsaidia mwalimu kuapngilia muda wake vizuri
4.Linatoa nafasi ya kufanya marekebisho ya mwelekeo wa ufundishaji
5.Linatoa nafasi kwa mwalimu mpya anayepokea vipindi kutoka kwa mwalimu mwingine
6.Linaonyesha njia, zana au vifaa atakavyotumia mwalimu katika ufundishaji na ujifunzaji
7.Husaidia kujua kasi ya ufundishaji mada kwa muda husika
 • Vipengele vya Azimio la Kazi/ scheme of work
1.Ujuzi/ competence
2.Malengo/ Objective
3.Mwezi/ month
4.Wiki/week
5.Mada kuu/main topic
6.Mada ndogo/sub topic
7.Vipindi/peroids
8.Vitendo vya ufundishaji/teaching activities
9.Vitendo vya ujifunzanji/ learning activities
10.Vifaa/zana/teaching aids/ materials
11.Rejea/ references
12.Upimaji/assessment
13.Maoni/ remarks/ recommendations
 • Katika uandaaji wa azimio la kazi kifaa muhimu cha kutumia ni muhtasari ambapo kuna vipengele mbalimbali vya azimio la kazi.
 • Kitu kinachotakiwa kuongeza ni kama vile maoni, wiki, upimaji n.k
 • Orodha hakiki.. Ni sehemu ambayo mwalimu anajaza kwa vile vitendo ambavyo mtoto anatakiwa aweze kuvifanya
 • Mkoba wa kazi
 • Fomu ya usahili
 • Mwalimu anapoandaa azimio la kazi ni muhimu awe mkweli kwa kuangalia uhalisia na hivyo si lazima kufuata mtiririko kama ulivyo katika muhtasari.
Andalio la somo
Mambo ya kuzingatia wakati wa maandalizi
1.Maarifa ya awali ya mtoto kuhusu mada ndogo
2.Malengo mahsusi kwa kila mada ndogo
3.Ubunifu na unyumbufu katika kuandaa na kutumia zana au vifaa vya kufundishia na kijifunzia
4.Kuchagua mbinu shirikishi zinazofaa kufundishia na kujifunzia
5.Muda wa ufundishaji wa mada ndogo
 • Muundo wa andalio la somo
-Jedwali la taarifa za awali
-Ujuzi/competence
-Mada kuu/ main topic
-Mada ndogo/sub topic
-Lengo kuu/ main objective. Lengo hili linaandikea kwa ujumla/wingi na mara nyingi haliwezi kupimika. Eg. Watoto waweze… should be able to…
-Lengo mahsusi/ specific obj. lazima liwe linapimika, (SMART). Wakati na baada ya kipindi cha dakika ishirini KILA MTOTO aweze….
-Zana/teaching materials
-Rejea/ references
 • Hatua za ufundishaji: safu wima tano
 • Hatua/stages. Kwa kutumia vifaa vya upimaji (observation). Kuchunguza kama…, kuangalia, kubaini kama watoto wanaweza … maswali hayatakiwi ila unaweza kujiuliza moyoni kama wameweza
 • Muda/time
 • Vitendo vya ufundishaji/ teaching activities
 • Viendo vya ujifunzaji/ learning activities
 • Vitendo vya upimaji/ assessment activities
 • Utangulizi/introduction
 • Maarifa mapya/new knowledge
 • Kukazia maarifa/reinforcement
 • Tafakuri/reflection
 • Hitimisho/consolidation
 • Tathmini ya mtoto/childrens evaluation. Wanafunzi 10 kati ya 20 wameelewa vitendo vituatavyo: kuorodhesha.. Tusiogope kubainisha. Hairihusiwi kuweka asilimia
 • Tathmini ya mwalimu/teachers evaluation
 • Maoni/remarks
Zoezi
Andaa Andalio la somo na Azimio la kazi