• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Mjadala kwa Wajasiriamali: Kuajiri ama kutoajiri ndugu wa karibu katika biashara zenu. Upi ni uamuzi sahihi na wenye manufaa (tija) zaidi?

Resha Mchanga

CEO & Founder
Staff member
#1
Habari Ndugu zangu Watanzania;

Kuajiri ama kutoajiri ndugu wa karibu katika biashara zenu. Upi ni uamuzi sahihi na wenye manufaa (tija) zaidi?
WANAOUNGA MKONO HOJA ya kuajiri ndugu wa karibu katika biashara zenu wanadai ya kwamba, ndugu yako akikuibia basi ile pesa inakuwa inazunguka mulemule katika ukoo wenu tofauti na kuajiri mtu wa mbali kisha akaiba na kupeleka pesa katika ukoo mwingine.

WANAOPINGANA NA HOJA ya kuajiri ndugu wa karibu katika biashara wanasema kwamba usipoajiri ndugu ndio kuna manufaa zaidi kwa maana ata akikuibia inakuwa ni rahisi zaidi kumfikisha katika vyombo vya sheria tofauti na ndugu wa karibu ambaye utamuonea aibu na vile vile ukoo mzima utakuweka kikao na kuanza kukusimanga kwanini unataka ndugu yako akaozee jela.

Upi ni uamuzi sahihi kati ya kuajiri ama kutoajiri ndugu wa karibu katika biashara? Na kwanini?
USISAHAU:
ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.


OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.