• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

MTANDAO WA FACEBOOK UMEIONDOA POST YA RAIS TRUMP

#1
Mtandao wa Facebook umeiondoa post ya Rais Trump huku mtandao wa Twitter ukiutaja ujumbe huo kama unaovunja kanuni za Twitter, ujumbe huo unasema mafua ya kawaida ni hatari zaidi kuliko corona, Trump ameandika hayo baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali alikokuwa anapatiwa matibabu baada ya yeye na Mkewe kuugua corona.

Trump aliandika>>”Msimu wa Watu kuugua mafua unakuja, Watu wengi wakati mwingine zaidi ya Laki moja bila kujali uwepo wa chanjo huwa wanakufa kwa mafua, swali ni je? tutaifunga tena Nchi yetu (lockdown)?, jibu ni hapana, tumejifunza kuishi nayo kama ambavyo tunajifunza kuishi na corona ambayo sio hatari sana ukilinganisha na mafua”