• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Mtu akikuomba ushauri kwa jambo kama hili utamjibu nini?

#1
KILA NIKIMUONA MTOTO WA MUME WANGU NAHISI KUCHANGANYIKIWA!

Kaka naomba tu unisaidie maana najikuta nashindwa haya maisha. Mimi nimeolewa ndoa yangu ina miezi minne sasa. Wakati nakutana na huyu mchumba wangu aliniambia kabisa kuwa ana mtoto ambaye amezaa na mwanamke mwingine, alishaachana na mwanamke na kaolewa hivyo yeye anaishi na mtoto wake kwani hataki mtoto wake kulelewa na Baba wa kambo.

Basi mimi sikua na shida, nilikua naenda kwake, namuona mtoto lakini wakati huo hata sikuona kuwa ni tatizo kwakua nilikua bado sijaolewa. Lakini Kaka baada ya kuingia kwenye ndoa, kuanza sasa kuishi na yule mtoto ndiyo sijui naonaje, mpaka nahisi kuchanganyikiwa. Katoto ni kakike, lakini ana sura ya Baba yake, yaani sijui nikuambieje Kaka, sio kwaba ni mtoto mabya, siwezi kusema hivyo lakini hatuendani naye kabisa.

Rafiki zangu wakija kunisalimia inabidi niseme tu ni mtoto wa ndugu yake na mume wangu lakini si mtoto wa mume wangu. Mtoto ana miaka mitano, ana akili, kachangamfu anajua kila kazi na ananiheshimu. Yaani kangekua katoto kazuri ningekapenda balaa kwani kana heshima sijui nikuambieje Kaka, lakini shida nashindwa, nikimuangalia wakati mwingine najiikuta na hasira tu nampiga hata bila sababu.

Hali hiyo inaniumiza kwani mwisho kanakuja kuniomba msamaha wakati hata hana kosa. Yaani kuna vitu vingine najikuta nagomba mpaka basi, nakua tu na chuki na mtoto. Wakati mwingine namfanyia visa tu ili kumpiga, mfano juzi nilimuwekea chakula kingi makusudi ili aache kula, basia liacha nikajikuta nampiga kuwa anachezea chakula basi nikamlazimisha kula na kweli alikula lakini alishindwa hata kunyanyuka yaani anapepesukapepesuka ila alimaliza na kuosha vyomboa akaosha.

Nilijisikia vibaya kwani sikupata faida yoyote, hali hii inanifanya nakua na kisirani, nakua mtu wa hasira hata kwa mume wangu. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, nataka kuongea na mume wangu amuondoe huyu mtoto ampeleke kwa Bibi yake. Mume wangu wazazi wake wamefariki lakini ana ndugu wengine, kuna Baba mdogo wake na wengine tu ambao wana uwezo.

Sio kama si mtaki moja kwa moja lakini aondoke tu ili niwe sawa maana nahisi naweza kumuua huyu mtoto. Shida ni kwamba mume wangu anampenda sana mtoto na kwakua yeye alilelewa na ndugu baada ya wazazi wake kufariki basi anasema kuwa mwanae hawezi kulelea na mtu mwingine yoyote na aliniambia kabla hata hatujaanza mahusiano, nisaidie kaka nifanye nini maana nahisi kuchanganyikiwa.

Je kama ni wewe ndio unaombwa ushauri kama huu, utamjibu nini, utamuacha salama kweli?