• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

MUONGOZO MFUPI WA KILIMO CHA MAHARAGE

#1
Habari mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu, Hapa Nitaelezea kwa ufupi kuhusiana na Kilimo cha maharage

Kilimo cha maharage ni rahisi na kinalipa sana kikifanyika kwa utaalamu na ufanisi. Gharama za kilimo cha maharage ni nafuu na ushindani wa zao sokoni sio mkubwa sana.
Mkulima Hahitaji kusafiri, kinachofanyika ni kuwaita wateja waje shambani kwake na kuchukua mzigo.

Ekari moja ya maharage ya njano kwa maeneo mengi huvunwa gunia kati ya 8 – 12 kutegemea na matunzo shambani.

Shamba la maharage ukilima kwa kumwagilia unaweza lima mara tatu kwa mwaka . Hii ina maana ukilima ekari moja tu utakua na uhakika wa kipato cha uhakika kila baada miezi 4.UOTESHAJI WA MAHARAGE

MBEGU
Upandaji wa maharage ufanyike katika muda muafaka kutokana na eneo ili kuweza kupata maji ya kutosha (mvua) na wakati wa mavuno kunatakiwa kuwe na ukavu ili maharage yasiharibikie shambani.

AINA ZA MBEGU
Kuna aina nyingi za maharage ambazo zinaweza kupandwa kwa mfano (Rojo, Mshindi, Pesa, SUA 90 na Canadian wonder) ambazo ni mbegu zilizoboreshwa.

KIASI CHA MBEGU KWA EKARI
Kilo 20 hadi 25 za mbegu za maharage zinatosha kuotesha shamba la ekari moja shamba,

UPANDAJI WA MBEGU


Namna ya upandaji wa mbegu za maharage

Inashauriwa kupanda maharage katika umbali wa sentimita 50 (mstari kwa mstari) na sentimita 20 (mmea kwa mmea), panda mbegu mbili za maharage katika shimo moja, mbegu zinaweza kupandwa katika umbali wa sentimita 3 Chini ya Udongo.
= ekari 2.471.

MBOLEA
Mimea ya maharage inahitaji virutubisho vya kutosha kutoka kwenye udongo ili kuweza kukua na kuzalisha matunda yenye afya.

Ni vizuri kutumia mbolea hai ambazo zinasaidia viumbe hai huweza kukua na kuendeleza kurutubisha udongo, kwa mfano mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen fixing bacteria) waishio kwenye udongo kutengeneza nitrogen.

Nashauri Mkulima kutumia mbolea ya DAP Kuoteshea maharage: DAP yaweza tumika kipindi cha kusia mbegu au wiki 1 mara baada mche kuota.

UDHIBITI WA MAGUGU
Shamba lililokuwa safi dhidi ya magugu

Inashauriwa kupalilia shamba mara tu magugu yanapotokea na kabla mimea haijatoa maua.

Palilia kwa jembe la mkono au kung'olea magugu na maotelea yote shambani, waweza tumia kemikali kudhibiti uotaji wa magugu kabla ya kupanda maharage shambani.

KUKABILIANA NA VISUMBUFU SHAMBANI

Maharage hushambuliwa na wadudu na magonjwa mbalimbali.
Miongoni mwa njia
za kuzuia, kukinga na kufukuza wadudu ni kuhakikisha kuwa mimea
ipo katika hali nzuri (imepaliliwa, nafasi ya kutosha na haijaharibika).

Pia kubadilisha aina ya mimea inayopandwa kwenye shamba moja mara
kwa mara husaidia kupunguza uwezekano wa wadudu kuongezeka.

KILIMO ANUAI (Organic Farming)
Kwa baadhi ya wadudu kama vile viwavi (African Ballworm) na magonjwa ya Fangasi huweza
kudhibitiwa kwa kutumia muarobaini au vitunguu saumu.

Maji ya muarobaini ni dawa nzuri sana kwaajili ya kufukuzia wadudu na kudhibiti magonjwa ya Fangasi na haina madhara yoyote kwa binadamu.

KEMIKALI: Tumia Viuatilifu kudhibiti magonjwa na wadudu wanaotokea shambani

VIUWA DUDU MADHUBUTI: Duduwill, Willcron, Cutter, Wiltigo, Liberate N.k

VIUWA KUVU (MAGONJWA YA FANGASI): wilthane,Superwill, Ridomil, Folicur n.k


MAHARAGE KUKOMAA NA KUVUNWA.
Maharage yaliyokomaa na kukauka vizuri

Maharage ya kijani/ Mabichi yanatakiwa yavunwe kabla punje za maharage hazijakuwa sana. Hii ni kati ya wiki 7-8 baada ya kupanda. Maharage makavu huvunwa mara tu kiasi cha kuridhisha cha kukomaa na kukauka kinapokuwa kimefikiwa.

Asilimia 80 ya maharage yakishakomaa na kuanza kubadilika rangi (kukauka) au kwa aina nyingine kusinyaa yanakuwa tayari kwa mavuno.

Kwa kawaida mmea wote hung’olewa na kuwekwa juani ili uendelee kukauka kisha maharage hutolewa kutoka kwenye mmea na kuendelea kukaushwa ili kupunguza matatizo wakati wa kuhifadhi.

Baada ya kukauka hadi kufikia angalaua asilimia 12 ya unyevu, maharage yanatakiwa yahifadhiwe kwenye chombo chenye mfuniko kama vile ndoo ya plastiki au pipa na kuendelea kuyaangalia mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa wadudu hawajaingia na kisha kuyafunika tena.

MAVUNO KWA EKARI
Magunia ya maharage sokoni

Maharage yakihudumiwa vizuri zaidi shambani hutoa mavuno ya Gunia kati ya 10-15 kwa ekari Moja

SOKO LA MAHARAGE.
jitahidi kutafuta na kufahamu soko la maharage kabla ya Kuanza kilimo cha maharage, Soko la maharage hutofautiana kulingana na msimu. Hivyo ni vyema Mkulima kufahamu soko lake kabla ya kuanzisha mradi.

Bei ya Gunia la maharage la kilo 120 huwa linauzwa sokoni kati ya 150,000/= hadi 200,000/= kutegemea na msimu wa zao sokoni.