• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Mzazi Aliyefaulu Vs Mzazi Aliyefeli

#1
Hii ndio lugha ya mzazi kwa mwanae aliefaulu kidato cha sita.

SAA 6:00 AM
BABA: Mwanangu, unaamka sasa hivi au unalala lala kidogo?

MTOTO: Hapana baba nimechoka nitaamka saa 5, jana nilichelewa kulala nilikua naangalia SCANDAL!!!

BABA: Haya baba basi kuna elfu 30 nimemuachia mama yako kama utajisikia kutoka utaitumia kama nauli.

MTOTO: Baba si uniachie zile funguo za rav4!!

BABA; Haina tatizo utaenda kuchukua pale chumbani kwangu usipoziona mwambie mama yako akupe, halafu sidhani kama hiyo pesa itakutosha kwa ajili ya mafuta upitie pale ofisini nikuongeze pesa.

Sasa hii ndio lugha kwa wale wa 4 na 0.

SAA 6:00 AM

BABA: We nguruwe umelala tuuuuuuu mpaka saa hizi hivi unajua bei ya hilo godoro??? Kazi kupata maziro tu kwa kulala lala lione, hebu amka unioshee gari niende kazini!