• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Njia 3 Za Ku ‘Reset’ Simu Ya Android!

#1Inafahamika wazi kuwa simu za Android kama vile Samsung Galaxy ndio wapinzani wakubwa wa kampuni Ya Apple ambao wana iPhone zinazotumia iOs. Watu wengi wanasema simu za android ni rahisi kutumia kuliko zile za Apple, Mimi nasema inategemea na mtu na chaguo lake (ha!). Watumiaji wa Android wanafurahia maelfu kwa maelfu ya aplikesheni (Application) zinazopatikana bure Google play.
Lakini kushusha aplikesheni nyingi katika simu yako inashusha kasi ya ufanyaji kazi wa simu yako, Je hili likitokea unafanyaje?. ikitokea hivi ni vizuri kureset simu yako, Lakini pia kureset simu yako kuna kanuni zake na zisipofuatwa unaweza jikuta unaharibu kifaa (simu) chako. Twende wote sambamba kuzijua njia tatu za kureset simu au tableti yako ya Android