• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Safari ya Rais Magufuli kwa barabara yawatumbua mameneja wa Tanroads Lindi na Pwani

#1
Waziri wa ujenzi mh Kamwele amewaondoa madarakani mameneja wa Tanroads wa mikoa ya Lindi na Pwani kufuatia kushindwa kuifanyia matengenezo barabara ya Dar hadi Mtwara.

Maamuzi hayo ya mh Kamwelwe yanafuatia maagizo yaliyotolewa jana na Rais Magufuli ya kutaka hatua zichukuliwe kutikana na ubovu wa barabara alioushuhudia kwenye takribani zaidi ya km 90 .

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!

=====

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Issac Kamwelwe ametengua uteuzi wa meneja wawili wa Wakala wa Barabara (Tanroas) wa Mikoa ya Lindi na Pwani kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ya kusimamia miundo mbinu ya barabara kwenye maeneo yao.

Uamuzi huo wa Waziri Kamwelwe umefanyika ikiwa ni siku moja tangu Rais John Magufuli alipopita kwenye barabra za mikoa hiyo akitoka mkoani Mtwara kuhudhuria maziko ya Rais mtaaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na kukerwa na uharibifu mkubwa wa barabara za mikoa hiyo.

Kamwelwe alichukua uamuzi huo jana alipokuwa akikagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye kilometa 1.6 inayotoka Kibaoni kwenda Makao Makuu ya Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoani Katavi.

Alikuwa njiani kutoka Mji Mdogo wa Inyonga uliopo wilayani Mlele kwenda mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Waziri Kamwelwe, mameneja aliotengua uteuzi wao ni Issac Mwanawima, Meneja wa Lindi na Yudas Msangi aliyekuwa Kaimu Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Pwani.

Waziri Kamwelwe alisema Rais Maguguli alipita juzi kwenye barabara hizo na kushuhudia lami ikiwa imeharibika na barabara imekuwa kama ya vumbi wakati zipo fedha za matengenezo kupitia Mfuko wa Barabara zipo.

Alisema Tanroads walikuwa na sifa nzuri lakini wameanza kuharibiwa na watumishi wachache. “Kwa hiyo watambue kuwa kipindi hiki siyo cha kufanya mchezo kila anayebainika kushindwa kutekeleza majukumu yake atambue kuwa atawajibishwa,” alisema.

Aliwataka mameneja wa Tanroads kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu barabara zote zilizoharibiwa na mvua za msimu huu zinakarabatiwa na zinakamilika.

Akifafanua, Kamwelwe alisema wizara yake imetoa zaidi ya Sh bilioni 35 kwa matengenezo ya barabara hizo na kwamba meneja atakayeshindwa kukamilisha, ajihesabu kuwa umeneja wake utaishia tarehe hiyo.

Alisema kabla ya kutoa agizo, aliwaita mameneja wa Tanroads wa mikoa yote kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma na kuwaelekeza wahakikishe wanafanya matengenezo ya barabara zote zilizoharibika kwa mvua za masika.