• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Serikali Msijisahau Katika Hili la Daktari Kumtibia Mtu wa Jinsia tofauti na Yeye

#1
MWakuu naomba niipongeze serikali kwa jitihada zake inazofanya katika kuhakikisha ile heshima ya jinsia zote inalindwa.

Tukiangalia katika majeshi hasa jeshi la polisi utakuta kuna askari wa kike ambao kama itatokea muhalifu ni mwanamke basi askari yule hakuajiriwa kwa bahati mbaya bali hiyo itakuwa ni kazi yake kumpekua sehemu za mwili wake.

Hali kadhaalika mwanaume atapekuliwa na askari wa kiume katika kulinda heshima.

Hata mashuleni kuna waalimu wa kike kibao ambao wao watashughulikia masuala mbali mbali ya wanafunzi wa kike.

Mbona sioni suala hili la kuheshimu jinsia na kulinda heshima ya mtu likifanyika na kusisitizwa katika kada ya afya ?

Kwa nini isiwe kosa daktari wa kumtibia mgonjwa wa jinsia tofauti na yeye ikiwa katika hospitali hiyo ama maeneo hayo kuna daktari mwenye jinsia sawa na mgonjwa ?

Kama ambavyo polisi haruhusiwi kumfanyia upekuzi wa mwili mtu wa jinsia isiyekuwa yake wakati wa jinsia yake wakiwa pale hii ni kosa,vipi isiwe kosa katika hii kada ya afya ?

Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.

Chumba cha kuzalisha kuna madaktari wa kike watano na wa kiume mmoja,huyu wa kiume anatafuta nini,kwa nini isiwe kosa kisheria?