• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

SHERIA ZA WANYAMA TANZANIA

#1
Tanzania imeadhimisha siku ya Veterinari duniani huku ikiwa bado inakabiliwa na changamoto ya Mamlaka ya Serikali kuvunja sheria ya Ustawi wa wanyama kwa kufanya vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanyama hao.

Miongoni mwa Misingi ya Ustawi wa wanyama inayovunjwa ni pamoja na Uhuru dhidi ya Kiu, Njaa na Utapiamlo, Uhuru wa kutojisikia vizuri, Uhuru dhidi ya maumivu, kuumizwa na magonjwa, uhuru wa kuonyesha tabia za asili pamoja na uhuru dhidi ya woga na msongo wa mawazo.

Siku ya Veterinari duniani huadhimishwa Jumamosi ya mwisho wa Mwezi Aprili kila mwaka ambapo Tanzania imeadhimisha April 28 kutokana na muingiliano wa siku ya kitaifa ya Muungano.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dk. Titus Kamani anasema licha ya kuwa na sheria ya Ustawi wa wanyama sura ya 154 ya mwaka 2014 lakini bado haitekelezwi ipasavyo.

Aidha wananchi pia hawajahamasika kuacha vitendo vya kikatili dhidi ya wanyama ambapo punda hubebeshwa mizigo kupita uwezo wao, huku wanyawa wakisafirishwa wakiwa wamebanana ndani ya buti za magari bila hewa ya kutosha.

Hata hivyo madaktari wa mifugo wanawajibu wa kusimamia misingi mitano iliyopo ya haki za wanyama.

Miongoni mwa mikakati ya maadhimisho ya sherehe hizo ni kuhakikisha kuna ustawi wa wanyama na binadamu.

Ni miaka 14 tangu kuanza kuadhimishwa kwa siku ya veterinari chini ya usimamizi wa Chama cha Madaktari wa Mifugo Duniani na Shirika la Afya ya Wanyama duniani ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni Ustawi wa Wanyama.