• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Skills 5 rahisi za kuwa nazo 2021

#1
1 • Uwezo wa kushawishi na kuclose deals kwa njia ya simu.

Wakuu niseme wazi ninaclose deals nyingi sana kwakutumia simu. Unajua siku hizi mambo mengi tunafanya kwakutumia simu zetu hizi sasa mimi binafsi nime master hii skill kwa maana ya kwamba ninauwezo wakumshawishi client/mteja kwa njia ya simu tu hata kama hatujawahi kuonana. Hii skill ni muhimu sana kwasababu kipindi hiki cha technology uwezekano ni kwamba unakuta mteja au client yupo sehemu ya mbali na wewe ulipo. Sasa mteja kama huyu hutakiwi kumpoteza, inatakiwa uwe mweledi wakufahamu namna gani utamshawishi kwa njia ya simu tu ili mwisho wa siku mkamilishe business mnayofanya.

Binafsi mimi nina formula nayotumia and it works like a magic. Ni wakati wako sasa kujifunza hii skill muhimu kabisa.

2 • Ujuzi wa kuandika kwa kushawishi.

Hivi unafahamu kwa huu uwezo pekee unaweza ukatengeneza pesa nzuri sana?

Niseme wazi tu nimeweza kuwafikia watu wengi sana lakini pia kuwashawishi watu hawa wakubaliane na ideas zangu kwa njia hii ya maandishi pekee. Wengi ya watu hawa walikuja kuwa paying customers wakinunua digital products nazouza au ku-promote.

Mtu wangu nikwambie kitu.

Hii skill ya kuweza kuandika kwa kushawishi itaendelea kuwa relevant hadi tamati ya maisha ya mwanadamu.

Kama ulikuwa unachukulia poa au unaona uvivu kuandika kuhusu biashara yako au hobbies unazozipenda nikwambie tu anza sasa hivi. Na kama unahitaji nikusaidie nipo hapa nitumie email. You will thank me later.

3 • Ujuzi wa kuweza kujifunza kwa haraka na kuelewa mambo kwa haraka.

Ok, najua nitakuwa nimekuchanga hapa.

Sivyo?

Kipindi hiki watu wengi si wazuri wakuweza kujifunza mambo kwa haraka na watu hawa wanadhani wao ni vilaza hawawezi lolote. Nop hiyo si sababu kabisa.

Ngoja nikwambie kitu. Kama ulikuwa unajifunza jambo fulani ukaona huwezi kuelewa kwa haraka basi ni muhimu kufahamu kwamba uwezo wa wewe kugundua huwezi kuelewa jambo hilo kwa haraka ni akili pia hiyo. Hapo cha kufanya inabidi utafute kitu kingine utachoweza kujifunza na kuelewa kwa haraka. It doesnt make sense unakuta mtu anajifunza kitu ambacho kamwe hatoweza kuelewa lakini bado anakosa utashi wakugundua yupo kwenye wrong track. Mtu huyu atapoteza muda aking'ang'ania kuendelea kujifunza na kamwe hatofanikiwa kwa lolote.

Mtu wangu nikwambie kitu.

Kuna vitu vingi sana unaweza kujifunza na ukaelewa kwa haraka. Hivi ndivyo unavyotakiwa kujifunza kwasababu dunia ya leo muda si rafiki kabisa. Ukikomaa muda mrefu kujifunza kitu au skill ambayo hutoelewa hata kama utatumia miaka na miaka huo ndiyo ukilaza wenyewe. Shtuka, jifunze skill au kitu utakachoweza kuelewa kwa haraka.

4 • Uwezo wa kusikiliza kwa umakini.


Siku hizi watu wanasikiliza au wanasoma kitu si kwa lengo la kuelewa. wengi wanasikiliza ili wajibu. Hii kitu sijui kwanini inakuwa hivi na ni jambo baya sana.

Unajua ukiwa na hii skill ya uwezo wa kusikiliza watu wngine iwe kwenye business au mambo mengine tu utaweza sana sana kutengeneza meaningful realtionship na watu na kama unavyofahamu ukijenga meaningful realtionship na watu wa maana basi jua soon deals zitaanza kukufuata.

Hapa naposema uwezo wa kusikiliza sisemi unasikiliza tu bila kufanya maongezi nop...inatakiwa pia ufahamu wapi unatakiwa kuongea au kuuliza swali au kupata clarification.

Mtu wangu nikusisitizie tena, hii skill pekee binafsi imenifanya niweze si tu kuwafanya watu naozungumza nao waone nina pay attention kwa wanachozungumza lakini pia wao nao huona umuhimu wa kunisikiliza pale napoongea. Kwa namna hii mazungumza yanakuwa deep lakini pia inajenga uaminifu na maelewano.

5 • Uwezo wa kufanya negotiation

Wakuu tunapoteza deals nyingi si kwasababu watu tunaofanya nao business hawana pesa au hawana nia nop.....sababu ni kwamba watu wengi hawapo vizuri kwenye negotiations.

Unajua maisha kila siku ni negotiations.

Mtu fulani akikwambia hataki kitu fulani hiyo haimaanishi hataki kabisa hiko kitu au niseme biashara unayojaribu kumweleza. Mara nyingi watu hawa ni kwamba hawakubaliani na baadhi ya mambo unayopendekeza, labda ni price, labada ni muda, labda ni umbali nk. Sasa ukiwa mjanja na umeona mteja anakataa deal unayo propose kwake basi utafahamu ni wakati wa kuanza negotiation kwa maana yakuanza kumshirikisha ili uone yeye anawaza nini. Hapa unakuwa umejiweka katika nafasi nzuri yakufanikisha deal yako kwasababu kwa kupitia negotiation mtaweza kufikia makubaliano. Kumbuka huitaji kuingiza hisia na kuanza kulalamika. Toa fact ili ueleweke.

Cheers