• Mpendwa, Wizara inapenda kuelekeza shule zote zenye Wanafunzi wa Kidato cha Sita naVyuo vyote vitakavyofunguliwa kuanzia tarehe 01/06/2020 kuhakikisha wanazingatia maelekezo vote kuhusu kujikinga na Virusi vya Corona.

Taarifa: Ofisi za HESLB Zahamia Temeke Vetenari, Dar Es Salaam.

#1
MA
NOTE: Taarifa Hii imetolewa na Tovuti ya HESLB

Tunapenda kuwafahamisha wadau wetu kuwa ofisi zetu za Dar es salaam zimehamia katika jengo la ‘HESLB House’ zilipokuwa ofisi za Wizara ya Kilimo katika eneo la ‘Temeke Veterinari’, Barabara ya Mandela, karibu na Makao Makuu ya TAZARA, Dar es salaam.

Hivyo shughuli na huduma tunazotoa zinapatikana hapo kuanzia Jumatatu, Machi 30, 2020.

Tunawashauri wadau wetu kuwasiliaa nasi kwa simu au barua pepe (0736 66 55 33, 0739 66 55 33 au info@heslb.go.tz)

Imetolewa Na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
HESLB House, 1 Mtaa wa Kilimo -TAZARA
Barabara ya Mandela,
S.L.P. 76068,
15471 DAR ES SALAAM, Tanzania
Barua pepe: info@heslb.go.tz