• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Tafakari; KIONGOZI BORA HUTOKANA NA MFUASI BORA

#1
Tafakari; KIONGOZI BORA HUTOKANA NA MFUASI BORA
Posted By ETETA media
2020-10-04
Zama zile kila kitu kilikuwa tofauti sana. Wakati na baada ya utumwa watu waliendelea kuathiriwa na mfumo mbaya ya kikoloni. Kama ni Kiongozi aliendelea kuenenda kama Nyampara, na kama ni mfuasi anayeongozwa aliendelea kujihisi kama mateka/mtumwa. Mmoja alijiita Meneja (Boss) na mwingine akaitwa mtumishi neno linalotokana na mtumwa. Kwakuwa wote waliamini katika utumwa, mambo yalikuwa shwari na maisha yaliendelea bila shida.
Katika zama za karne ya 21, mambo yamebadilika. Mwelekeo mpya ni kufanya kazi kama timu (Team work) baina ya kiongozi na wafuai wake. Pamoja na kwamba kila taasisi inakuwa na kiongozi Mkuu, kila mmoja anatakiwa kubadilika kulingana na hali inayoendelea. Wakati fulani awe kama kiongozi na wakati mwingine awe kama mfuasi. Wakati mwingine inatakiwa kusiwe na kiongozi wala mfuasi bali wote walingane/wafanane ili wafanye kazi kama wachezaji wa timu moja.
Si wakati wote unatakiwa kuwa mwalimu, wakati mwingine jaribu kuwa mwanafunzi. Hii ni kwa sabau hakuna anayejua kila kitu na hakuna asiyejua kila kitu.
Unaposikia kwamba taasisi fulani haina huduma nzuri, haiendelei, inapata hasara, haina wafanyakazi mahiri, haifai nk; inatokana na sababu moja kubwa kwamba wanataasisi wameshindwa kucheza kwenye nafasi zote mbili. Wanalazimisha kuendana na zama ambazo wakati wake umeshapita. Kiongozi analazimisha kuwa kiongozi wakati wote na mfuasi analazimisha kuwa mfuasi wakati wote. Kila upande unaishia kutupia lawama upande mwingine bila kujua mzizi wa tatizo. Matokeo yake kiongozi anakosa wafuasi; wafuasi nao wanakosa kiongozi wa kumfuata. kila kitu kinakuwa kivyake vyake; “things falls apart
Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama si mfuasi mzuri, na huwezi kuwa mfuasi mzuri kama si kiongozi mzuri.
Ukikubali Wajibu, Timiza Wajibu!​