• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

TAHLISO Yaridhishwa na Maendeleo ya Miradi Jijini Dodoma

#1
Kamati Kuu Tendaji ya TAHLISO Imefanya Ziara ya Kutembelea Miradi Mbalimbali ya Maendeleo Jijini Dodoma.
IMG-20200330-WA0045-450x530.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi akisalimia na Mwenyekiti wa TAHLISO Ndg. Peter Niboye.

Kamati Kuu Tendaji ya TAHLISO Ikiongozwa na Mwenyekiti Ndg. Peter Niboye Wametembelea Miradi Mikubwa ya Kimkakati Inayojengwa kwa Kutumia Pesa Kutoka Serikali Kuu Ikiwemo Mradi wa ‘Bus Terminal’ Wenye Gharama ya Zaidi ya Billion 24, Soko Kuu Linagharimu Shilingi Billion 14 Pamoja na Chinangali ‘Recreation Centr’ (Bustani kwaaajili ya Mapumziko) Imegharimu Shilingi Bilion 2.9.

IMG-20200330-WA0027-705x470.jpg

Wajumbe wa Kamati Kuu Tendaji ya TAHLISO wakipewa mafunzo kwenye moja ya mradi waliotembelea.

Kamati Kuu Tendaji ya TAHLISO kwa Pamoja Wameipongeza Serikali Inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pamoja na Wasaidizi Wake Wote kwa Kusimamia Vyema Utekelezaji wa Miradi hii ya Kimkakati.

IMG-20200330-WA0022-705x470.jpg

Wajumbe wa Kamati Kuu Tendaji ya TAHLISO wakiwa kwenye matembezi ya mradi.
Ziara Hii ya Kimkakati Jijini Dodoma Imehusisha Viongozi Mbalimbali Wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi.

IMG-20200330-WA0024-705x470.jpg

Wajumbe wa Kamati Kuu Tendaji ya TAHLISO wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya mradi.

Ziara Hii ni Muendelezo wa Vikao Kamati Kuu Tendaji kwa ajili Maandalizi ya Mpango Kazi wa Mwaka mmoja.
 
Last edited: