• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Tujifunze hapa namna ya kutengeneza Android Apps A-Z

#1
Katika thread hii tutajifunza namna ya kutengeneza application za Android "from the scratch", Japokuwa kuna "platforms" mbalimbali mtandaoni ambazo zinaweza kumsaidia mtu yoyote kuunda apps hata pasipo kuwa na ujuzi wowote kuhusu programming, hapa itakuwa ni tofauti.

Imani yangu wale wote ambao watakuwa na mwamko wa kujifunza kuunda apps za Android ni kwamba wana ufahamu wa kufanya programming kwa kutumia JAVA ama OOP language yoyote na pia wana uelewa hata kidogo kuhusu xml (Extensible Markup Language).

Mtindo ambao tutajifunza ni kwa namna ya ku-develop projects (apps) mwanzo mwisho, na tutakopofika ukingoni mwa mafunzo haya ningeomba tushirikiane kwa pamoja kuunda app ambayo itakuwa nzuri na kisha tuunde hata team ambayo tutaweza kuunda apps mbalimbali.

Zifuatazo ni projects ambazo tutazifanya kupitia uzi huu:

1. Welcome App
2. Android Media Player
3. Tip Calculator App
4. Music Event App
5. Uber Clone
6. Messaging App (Whatsapp Clone)
7. Flag Quiz App
9. Cannon Game App
10. Weather App
11. Media, Videos and Sound Apps
12. Instagram Clone

Karibuni nyote.
 
#2
SEHEMU YA KWANZA: MAHITAJI(TOOLS) YA KUWEZA KUFANIKISHA UUNDWAJI WA ANDROID APPS
Kuna programu kadhaa ambazo zinahitajika ili kuweza kuunda hizi apps, programu hizo ni kama zifuatazo.

1. kompyuta inapaswa iwe na JAVA Development kit (JDK),
Apps za android kwa asilimia kubwa huundwa kwa kutumia java hivyo ni vizuri ukapata SDK ya javaa ambayo ni latest kabisa, unaweza kuipata kwa kutumia link ifuatayo,
Java SE Development Kit 8 - Downloads

2. Android SDK ambayo imeambatanishwa na Android Studio IDE
Hizi tooks zipo kwa ajili ya platform(OS) tofauti tofauti, kwangu mimi nitakuwa natumia windows na si linux lakini ukitaka kwa upande wa linux pia zipo.
Android Studio ndio ambayo tutaitumia katika kuandika codes, hii ni IDE rasmi ya android kwani zamani Eclipse IDE ndio iliyokuwa inatumika.
links.
kwa ajili ya windows,
Download Android Studio and SDK Tools | Android Studio