• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Umuhimu wa Kunywa Maji Baada ya Tendo la Ndoa

Wanachuo Doctor

WF Doctor
Staff member
#1
Utafiti mpya wa kisayansi uliochapishwa nchini Scotland umeelezea umuhimu wa kunywa maji baada ya tendo la ndoa kwa sababu unawakinga wanandoa husika dhidi ya kuumwa kichwa na tatizo la ukavu, na kwamba maji ni miongoni mwa funguo za furaha ya ndoa.

Utafiti huo umeonesha kuwa kutokunywa kiwango cha kutosha cha maji huwa na athari kwa afya jumla ya mwili na kusababisha mhusika kupatwa na maradhi mbalimbali.

Imebainishwa kuwa asilimia 40 ya wanandoa wasiokunywa kiwango cha kutosha cha maji baada ya tendo la ndoa, hupatwa na tatizo la kuumwa kichwa na kukosa shauku. Hali hiyo inapoendelea huwafanya wote wapatwe na tatizo la ukosefu wa hamu.

Hilo linatokana na kwamba ndani ya nusu saa ya tendo la ndoa mwili hutumia nguvu sawa na kukimbia umbali wa kilometa 4.

Mshauri wa chakula tiba, Maha, amesisitiza kuwa baada ya tendo la ndoa hitajio la vimiminika huongezeka, na akashauri kutumia chakula chenye maji kama chanzo cha asili kama vile juisi ya matunda na kadhalika.

Wataalamu wanashauri kuwa kuna umuhimu wa kunywa glasi 8 za maji kila siku. Hii ni kanuni ya kitiba ambayo baadhi ya watu wanaijua lakini wengi wanaipuuza. Kiwango hicho ni sawa na kiwango cha maji ambacho mwili unakipoteza ndani ya siku moja kupitia njia mbalimbali kama vile kupumua, kukojoa na kutokwa na jasho. Hivyo, kiwango hicho kinapaswa kurudishwa ili mwili usipatwe na hali ya ukavu na ukosevu wa hamu.