• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Umuhimu wa tovuti/mtandao kwa biashara ndogo.

#1
Katika ulimwengu wa leo kupatikana au kutokupatika kwa biashara yako katika mtandao wa internet kutaathiri kiasi cha mafanikio utakayopata. Ni muhimu kila mmiliki wa biashara kuwezesha biashara yake kupatikana na kuonekana mtandaoni kwa kupitia tovuti za kompyuta,simu au kurasa za mitandao ya jamii. Mtandao wa internet unatakiwa uwe nguzo na nyenzo muhimu sana katika mkakati wako wa kutangaza biashara au bidhaa.

Katika sehemu ya kwanza ya makala hii nitaonyesha umuhimu wa mfanyabiashara au mtu binafsi kumiliki tovuti. Tovuti nzuri ina uwezo mkubwa wa kuipa biashara yako thamani na kukutofautisha na washindani wenzako katika soko la bidhaa na huduma.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za kumiliki tovuti na kuitumia kama chombo cha kufanya biashara na kujitangaza.
Tovuti itafanya biashara yako iaminike zaidi.

Katika kizazi hiki watu wengi zaidi hutegemea mtandao wa internet kutafuta taarifu kuhusu bidhaa au huduma flani kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Biashara yako itanufaika mno kama itakua inapatikana kwa urahisi mtandaoni. Bila tovuti wateja wengi hasa vijana watafanya manunuzi kwa washindani wako ambao taarifa zao zinapatikana mtandaoni.

Utajitangaza saa 24 kila siku kwa gharama kidogo kuliko njia nyingine za kawaida za matangazo.
Gharama ya kutengeneza tovuti hutofautiana kulingana na mtengenezaji lakini punde tovuti itakapo kamilika, itakupa wewe na biashara yako uwezo wa kujitangaza kila saa sababu tovuti hupatikana hewani muda wote,wakati wowote na mahali popote ulimwenguni. Njia za kawaida za kujitangaza kama redio,magazeti na TV zinagharama kubwa mno. Tovuti iliyotengenezwa vyema ni moja kati ya njia rahisi zaidi na ya gharama nafuu zaidi ya kutangaza biashara yako katika kizazi hiki kinachotegemea mtandao.

Tovuti ni kipeperushi chako cha mtandaoni.
Tovuti ni kipeperushi kinachoelezea biashara yako ambacho kinaweza onekana mahali popote duniani. Vipeperushi vya kawaida huchanika na kuharibika baada ya muda lakini tovuti huzidi kuonekana pasipo kujali ilitengenezwa lini. Tovuti pia ni njia rahisi ya kuwataarifu wateja wako kuhusu bidhaa mpya,promosheni au huduma mpya.

Urahisi kwa wateja wako
Tovuti huwapa wateja wako urahisi mkubwa, kwa sababu wanaweza wakatafuta/kugundua bidhaa na huduma ulizonazo wangali nyumbani au ofisini mwao pasipo kuingia gharama ya kusafiri hadi dukani mwako. Urahisi huu huwasaidia wateja wako kuokoa gharama na hivyo kuvutiwa zaidi kufanya biashara na wewe. Wateja huvutiwa kwa sababu miundo mbinu yako huwasaidia kupunguza gharama ambazo wangekabiliana nazo kutembelea duka lako ili kujua huduma na bidhaa zipatikanazo. Swala hili litakupa upendeleo machoni pa wateja kuliko wenzako wasio na miundo mbinu ya mtandaoni.

Uwezo wa kufanya biashara popote nchini na ulimwenguni.

Tovuti hupatikana popote ulimwenguni, kwa hivyo unaweza kupata wateja popote pasipo kujali mipaka ya kijiografia. Unachotakiwa kufanya ni kutoa huduma na bidhaa ambazo ni bora kuliko washindani wengine katika soko husika.
Ni muhimu SANA kwa mmiliki wa biashara kutengeneza tovuti au ukurusa katika mitandao ya kijamii kwani uwepo wako mtandaoni utachangia sana kukuza kipato chako hasa katika bidhaa na huduma zinazotumika na vijana.

***

Tunaweza kutengeneza tovuti kwa ajili ya biashara yako kwa gharama nafuu. Wasiliana nasi kwa:

Simu / SMS/ WhatsApp: +255 711 414 246