• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Vidokezo 5 vya kufanikisha urembo halisi! Kwa KILA msichana.

Edgar Mbele

Moderator
Staff member
#1
Vidokezo 5 vya kufanikisha urembo halisi!
Kwa KILA msichana.

Ninajihisi mrembo ninapojiamini, ninapokuwa mwenye nguvu na ninapoweza kukabiliana na mambo yote. Nilivyokua, mwili wangu ulipitia mabadiliko mengi ya kihisia na ya kimwili, ilikuwa rahisi kusahau urembo wangu.

Lakini niliweza kupata njia ya urembo halisi na niko tayari kushiriki siri zote nawe. Siri kubwa ni ipi? Tayari una mambo yote unayohitaji!

Kubali tofauti zako

Nilikuwa naona aibu juu ya madoa niliyokuwa nayo usoni, kwani hakuna rafiki yangu aliyekuwa nayo.. Kila nilipozidi kukua, niligundua kwamba maumbile ya kipekee ya kila mtu ndiyo yanayowafanya warembo.

Siwezi kubadilisha ninavyoonekana – siwezi kujirefusha au kubadilisha rangi ya macho yangu. Lakini siyo lazima. Kila mtu ni tofauti na utofauti ni urembo!

Wewe pekee ndiyo unaweza kufafanua urembo

Majarida na mtandao unaonyesha wazo dogo kuhusu urembo. Badala ya kuangalia pale, angalia karibu nawe ili uone urembo halisi. Angalia kwenye kioo au watu karibu nawe. Siyo ngozi kamili au meno yanayowafanya watu kuwa warembo – kinacho watofautisha watu ni jinsi walivyo wacheshi au jinsi walivyo marafiki wazuri!

Uliza watu wengine

Ni rahisi sana kusahau mambo yanayotufanya kuwa warembo. Wakati mwingine – unahitajika kumwambia mtu mwingine akukumbushe. Niliwauliza marafiki zangu ni nini kirembo na wakasema, tabasamu langu la mzaha, jinsi kicheko changu ni kikubwa na jinsi ninavyo wakumbatia kwa uchangamfu.

Jipende kwanza

Mafuta mapya ya kujipaka uso au kujipodoa siyo siri ya urembo. Urembo halisi unaanza kwa kupenda mwili wako. Kama tu kinachohitajika na maua ili kustawi – mwili wako unahitaji kiwango sahihi cha maji, jua na virutubishi. Kula kinachokufanya uhisi vyema na kunywa maji ya kutosha – utang’aa!

Toa jasho

Ninahisi mrembo zaidi baada ya kukimbia – hata kama uso wangu umekuwa mwekundu na nimefunikwa na jasho. Ninahisi mwenye nguvu na mzima wa afya. Kufanya mazoezi hujaza mwili wako na homoni za furaha na inakusaidia kujihisi mrembo kwa ndani na pia bora zaidi nje. Tafuta mchezo au zoezi linalokufanya uhisi mwenye nguvu!