• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Waingereza wanafanya mapenzi kwa kiwango kidogo tofauti na miaka ya nyuma

#1
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Siku za hivi karibuni imegundulika kuwa waingereza wanafanya mapenzi kwa kiwango kidogo tofaiti na miaka ya nyuma , kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika taifa hilo.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la 'British Medical' , a,mbapo umesema kuwa tatu ya nne ya wanawake na wanaume hawajafanya mapenzi mwezi uliopita.

Idadi hiyo imeongezeka kwa takribani moja ya nne tangu mwaka 2001, kwa mujibu wa takwimu ya watu 34,000.

Zaidi ya nusu ya wanaume na wanawake wenye umri wa kati ya miaka 14 mpaka 44 wamefanya mapenzi wiki iliyopita, ripoti hiyo inaeleza.

Wapenzi wanaoishi pamoja au wanandoa , kiwango cha kufanya mapenzi kimeshuka zaidi.

Kupungua kwa ngono
Taarifa ambazo watafiti wameziangalia zimetoka kwa tafiti tatu zilizofanikiwa kufanywa na watafiti wa kitaifa wa nchini humo kuhusu tabia za watu na ushiriki wa ngono zilizofanywa mwaka 991, 2001, na 2012 .

Utafiti huo umetoa picha ya namna waingereza wanavyojihusisha na ngono.

Kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni:

  • Asilimia 41 ya watu wenye umri kati ya miaka 16 mpaka 44 huwa wanafanya mapenzi angalau mara moja kwa wiki mwezi uliopita
  • Uwiano wa ripoti wa watu kutoshiriki katika ngono katika mwezi uliopita imeongezeka kutoka asilimia 23 mpaka asilimia 29 miongoni mwa wanawake huku wanaume imeongezeka kutoka asilimia 26 mpaka 29.2 kati ya mwaka 2001 mpaka 2012
  • Idadi ya watu walioripotiwa kujihusisha na ngono mara kumi au zaidi imepungua mwezi uliopita kutoka asilimia 20.6 kufikia 13.2 kwa wanawake huku wanaume kiwango kikiwa kimeshuka kutoka asilimia 20.2 mpaka 14.4 kati ya mwaka 2001 na 2012
  • Wastani wa idadi ya watu wenye umri wa miaka 35 mpaka 44 kufanya mapenzi mwezi uliopita imepungua mwezi uliopita kutoka mara nne na kufikia mara mbili kwa wanawake na kwa wanaume imepungua kutoka mara nne mpaka mara tatu.
Kwa nini ngono imepungua?

Watafiti kutoka shule ya usafi na madawa ya kitropiki unasema kiwango cha ushiriki wa ngono wa mara kwa mara miongoni mwa watu ambao walikuwa wanafanya mapenzi kila wakati umepungua tofauti na idadi ya watu kuamua kuendelea kuhifadhi ubikira wao .CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ingawa watu wenye umri chini ya miaka 25 na wale ambao hawana wapenzi wanaonekana kuwa na unafuu katika kushiriki katika ngono, kiwango kimeshuka kwa wanandoa na watu wenye umri mkubwa au wapenzi wanaoishi pamoja kwa muda mrefu.

Je, hii ina maanisha kuwa watu wataacha kabisa kufanya ngono? Haiwezekani.

Nusu ya wanawake na karibu ya 2/3 ya wanaume katika utafiti uliopita walisema kuwa wangependa kufanya mapenzi zaidi.

"Hamu ya kufanya mapenzi zaidi ilisikika kutoka kwa watu ambao wako katika ndoa au wapenzi wanaoishi pamoja", watafiti walisema , "wanahitaji pongezi".

Kuwa na kazi nyingi na msongo wa mawazo?

Mtafiti aliyeongoza utafiti huo, Profesa Kaye Wellings alisema kasi ya maisha ya kisasa inaweza kuwa sababu ya watu wengi kutofanya ngono kwa kiwango stahiki.

Kinachoshangaza ni kuwa wale ambao wanaathirika zaidi ni watu wenye uwezo wa wastani katika maisha.

"Hawa ni wanawake na wanaume ambao mara nyingi wanapambana kazini, kuhudumia watoto na wana majukumu ya kuwatunza wazazi wao ambao wamekuwa wazee sasa."

Inawezekana shinikizo kubwa kutoka katika matokeo ya utafiti juu ya ngono unaweza kubadili mtazamo,

Huku usawa wa kijinsia unashauri wanawake kuwa wepesi kukutana na wenza wao ili kukidhi mahitaji yao ya wapenzi wao, wasema watafiti

Jambo lingine ambalo linaweza kuwa limepunnguza vitendo vya ngono ni ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii.

"Kufanya mapenzi kwa kiasi si jambo baya mara zote", Profesa Wellings alieleza.

Aliongeza kuwa matokeo ya utafiti yanapaswa kupokelewa chanya na wengi.

"Ni jambo gani muhimu kwa watafiti si kujua mara ngapi watu wanafanya mapenzi lakini kwa nini ni muhimu kujua kutoshiriki kwao.

Watu wengi wanaamini kuwa watu wengine huwa wanafanya mapenzi mara kwa mara kuliko wengine.

Watu wengi wanataka kunapenda kubaini wasiwasi wao kama hawako nje ya mstari ."

Jambo la muhimu ni ubora sio wingi. Kama wanafurahia kile walichokipata kuna uwezekano mkubwa wa utafiti huo kufanyika tena.

Lakini jambo la muhimu ni kwamba watu wanapaswa kutenga muda wa kufanya ngono, itawasaidia zaidi