• Mpendwa, Jiunge na Jamii ya Wanafunzi Kwa Kujisajili au Login Kama Tayari ni Member. Endelea Kuchangia Mada, Kuanzisha Mijadala Mbalimbali na Ujishindie Zawadi kutoka kwetu. Kama Simu, Laptop, Vocha na Nyinginezo Nyingi.

Yajue madhara ya kunyonyana Viungo vya Uzazi Wakati wa Tendo la Ndoa (Oral sex)

Wanachuo Doctor

WF Doctor
Staff member
#1
MADHARA YA KUNYONYANA WAKATI WA TENDO LA NDOA. ( Mapenzi yanayohusisha mdomo na viungo vya uzazi)
Kwa sasa katika jamii asilimia kubwa imeathiriwa na tamaduni hii ya wapenzi kuridhishana kwa njia ya kunyonyana sehemu za siri ambayo kiuharisia huhatarisha afya zao.

Tabia hii imeigwa katika video za ngono kutoka ughaibuni hasa kwa wazungu wanaofanya biashara za video za ngono, watu bila kujua kwamba wanaofanya video za ngono wapo kikazi na ni biashara yao, hivyo kabla ya kufanya hivyo huaandaa mazingira ambayo yatawafanya wawe salama kiafya wanapocheza video hizo mfano kupima afya, wahusika hupima magonjwa yote yanayohusisha viungo vya uzazi, na magonjwa mengine yanayo ambukiza na kuzingatia usafi ndipo huanza kuigiza video hizo.

Sasa wanaoiga michezo hiyo kwa bahati mbaya hawahusishi kabisa vipimo wala kujua afya zao zikoje matokeo yake huwa katika hatari kubwa ya kupata magojwa.

HAPA NIMEKUANDALIA BAADHI YA MAGONJWA AMBAYO UNAWEZA AMBUKIZWA KIRAHISI UNAPOFANYA MICHEZO HIYO YA KUNYONYANA.

1. 👉Gonorrhea
Hili huanzia katika koo la muambukizwaji, na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadae hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi na kuanza kuonyesha dalili.

2. 👉Syphilis
Huu huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotokea mdomo ukakutana na kiungo chenye athari hizo.

3. 👉Chlamydia
Huu pia huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalali kwa muda mrefu Ni ugonjwa unaoweza kuupata na ukadumu nao kwa muda mrefu.

4.👉hepatitis A
Huyu ni Virus anayepatikana katika kinyesi cha binadamu, huyu huwaingia wale wanaopenda kunyonyana na kulambana sehemu za haja kubwa.

5. 👉Hepatitis B
Huu huambukizwa kama HIV (virusi vya ukimwi) vile maana virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za siri na damu Na huu Ni ugonjwa unaoenea kwa kasi sana kwa sasa na kasi hii ya ueneaji inatokana na kuongezeka kwa tabia hizi za kunyonyana katika via vya Uzazi.

6. 👉Hepatitis C
Huu hupatikana pindi damu inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu!

Yapo Madhara Mengine mengi kama kansa ya Koo ambayo kwa sasa limekua janga kwa wanaume wengi sana na miongoni mwa Sababu zinazotajwa kusababisha zaidi ni tabia hizi za kuzama chumvini. nimezungumzia haya machache ili nisikuchoshe msomaji wa makala hii.

Kazi ni kwako chagua kipi bora utamu au kupatwa na magonjwa hayo hatarishi